Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 15, 2010

20 JUNI KUADHIMISHWA SIKU YA WAKIMBIZI DUNIANI


Wakilishi wa UNHCR B. Oluseyi Bajulaiye akizungumza na waandishi wa habari juu ya maadhimisho ya siku ya wakimbizi Duniani yatakayofanyika 20 juni kulia ni Naibu Mwakilishi, Bi Chansa Kapaya
Naibu Mwakilishi Bi.Chansa Kapaya
Mwakilishi wa shilika la UNHCR Bw.Oluseyi Bajuiye akiongea na waandishi wa habari leo kuhusu mahadhimisho ya siku ya wakimbizi duniani itakayofanyika juni 20 2010Kupata Makazi – Tanzania yaadhimisha Siku ya Wakimbizi Duniani

Tarehe 20 Juni, Siku ya Wakimbizi Duniani, kauli mbiu ya dunia ikiwa
“Makazi”, UNHCR pamoja na Serikali ya T
anzania, washirika na
wafadhili wake wanaanda shughuli mbali mbali kutambua suluhu
zilizopatikana kwa maelfu ya wakimbizi nchini Tanzania na kubainisha
magumu na nguvu z
a wakimbizi waliobaki ambao makazi ni kumbukumbu ya
mbali

Maadhimisho mkoani Rukwa na Tabora yatalenga kupewa uraia hivi
karibuni
kwa wakimbizi 162,000 kutoka Burundi, ambao wamepewa hifadhi tangu
mwaka
1972 kwenye “Makazi ya Muda Mrefu” ya Katumba, Mishamo na
Ulyankulu.
Matukio yanayo jumuisha Watanzania wapya na jamii za wenyeji ni pamoja
na tamasha za kimila, mashindano ya baiskeli na uzinduzi wa maboresho
ya
Shule ya Sekondari ya Tabora, ambayo yamefanyika hivi karibuni. UNHCR
pamoja na jumuiya ya kimataifa walifadhili upanuaji wa shule hii ya
kihistoria ya Sekondari, katika juhudi za kuwawezesha raia wapya
kujumuika kwa urahisi

Tangu mwaka 2005 Serikali pia ilitoa uraia kwa kundi dogo la
wakimibizi
Wakisomali wenye asili ya Kibantu wanaoishi na kufanya kazi kwenye
makazi ya Chogo, mkoani Tanga, ambapo walipata makazi mapya kwenye
ardhi
ya mababu zao.

Kwenye maadhimisho ya Siku ya Wakimbizi Duniani UNHCR ikishirikiana na
Alliance française wanaanda maonyesho ya picha yanayoonyesha hatua kwa
hatua jinsi hawa Wasomali wa zamani wanavyojumuika katika jamii ya
Watanzania na sherehe zao za kipekee za kitamaduni. Uzinduzi wa
hadhara
wa maonyesho haya, yakipambwa na ngoma za kienyeji kutoka mkoa wa
Tanga, utafanyika Jumanne tarehe 22 Juni saa 12.30 jioni.

Kupitia shughuli hii UNHCR pamoja na washiriki wake wanataka kutambua
juhudi za Serikali ya Tanzania katika kuwatafutia na kuwapatia
wakimbizi
suluhisho za heshima na za kudumu. Lakini pia tunataka kubainisha
magumu
na nguvu za wakimbizi 37,000 kutoka Burundi na 59,000 kutoka Kongo
waliobaki kwenye makambi mkoani Kigoma ambao makazi ni kumbukumbu ya
mbali.


Mnamo mwaka 2000, Tanzania bado ilikuwa inahifadhi takriban wakimbizi
680,000 kwenye makambi katika mikoa ya Kigoma na Kagera, ikiwakilisha
idadi kubwa kabisa ya wakimbizi barani Afrika. UNHCR iliwasaidia wengi
wa wakimbizi hawa kurejea nyumbani na, leo, kambi mbili tu zimebaki
moja
ikiwa ya Wakongo na nyingine ya Warundi. Kutokana na hili, UNHCR
kidogo
kidogo inapunguza uwepo na shughuli zake katika eneo hili la nchi huku
ikiendelea kutoa hifadhi na kusaidia wakimbizi waliobaki, ikilenga
makundi yalioko katika hali hatarishi.

Pamoja na kwamba nafasi ya Tanzania kama nchi ya hifadhi ilishuka
kutoka namba 7 hadi namba 21 mwaka 2009, idadi ya watu waliolazimishwa
kuhama makazi yao duniani inaongezeka. Kutokana na ripoti ya UNHCR ya
Global Trends, ambayo inazinduliwa leo, watu milioni 43.3 walihamishwa
kutoka kwenye makazi yao kutokana na mapigano na mateso mwishoni mwa
mwaka 2009, idadi ilioko juu kabisa tangu katikati ya miaka ya 1990.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...