Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 22, 2010

FAMILIA YA WATU SABA YATEKETEA KWA MOTO MBEYA

Na Moses Ng’wat,
Mbeya.

WATU saba wanaodaiwa kuwa wa familia moja katika mtaa wa Soweto jijini Mbeya,wamepoteza maisha baada ya nyumba yao walimokuwa wamelala usiku kuteketezwa kwa moto.

Habari za awali zilisema zilizothibitishwa na majirani wa familia hiyo zinadai kuwa moto huo mkubwa uliozuka ghafla usiku wa jana majira ya saa sita usiku katika nyumba hiyo yenye vyumba saba na kusababisha maafa hayo.

Habari zaidi zinadai kuwa tukio hilo liligunduliwa na walinzi walio kuwa karibu na nyumba hiyo baada ya kuona moshi mkubwa juu ya paa la nyumba hiyo kasha kuanza kupiga kelele za kuomba msaada.

Inadai kuwa kelele za mlinzi huyo zilliwaamsha majirani ambao walifika haraka katika eneo la tukio na kuanza jitihada za kuwaokoa watu waliokuwemo ndani kwa kuvunja milango na madirisha.

Mmoja wa jirani hao aliyejitambulisha kwa jina la Oscar, alisema baada ya kuvuja mlango vijana wawili walijitosa ndani ya chumba kimoja ambao walikuta miili ya watu watatu wakiwa ndani ya chumba kimoja wakiwa wamekufa na miili yao imeungua vibaya.

Alisema wakati jitihada hizo za kuwaokoa wanafamilia hao zikiendelea walipiga simu polisi ili kuongeza nguvu kwa kuwa moto huo uliendelea kuwaka katika sehemu ya nyumba hiyo, na kwamba muda mfupi polisi walifika wakiwa kwenye gari namba za usajili PT O944 aina ya ‘Landrover Defender’ na kuchukua majeruhi na miili ya marehemu na kuwakimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

Mbali na polisi pia kikosi cha kilidaiwa kufika mapema katika eneo la tukio ,lakini kwa bahati mbaya walikuta moto huo umeshasababisha madhara makubwa ,ikiwemo kusababisha vifo vya wanafamilia hao.

Mmoja wa askari hao wa zimamoto ambaye cheo chake hakikuweza kufahamika mara moja Mohamed Said, alisema walipata taarifa za moto huo baada ya kupigiwa simu na Polisi na ndipo walipoondoka haraka kukimbilia kwenye eneo la tukio.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa miongoni mwa watu saba waliofariki, wamo wanafunzi watatu waliokuwa wakisoma shule mbalimbali mkoani hapa.

Nyombi, aliwataja waliokufa katika tukio hilo la kusikitisha kuwa ni baba wa familia hiyo Daniel Mwang’ombe (75), Enith Richard (46)
Ambaye alikuwa mke mdogo.

Wengine waliokufa katika ajali hiyo ni Salome Mwang’ombe (18), Jenny Samson (10), Diana Samson (18) wote wanafunzi, Claud Samson (4), ambapo mtu mmoja jina lake halikupatikana.

Alisema chanzo cha moto huo bado hakijafahamika na kuwa Polisi wananendelea na uchunguzi zaidi na kwamba miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Rufaa Mbeya.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...