Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 16, 2010

Ligi ya Copa Coca-Cola kuanza Ijumaa


Na Victor Mkumbo

MABINGWA watetezi wa michuano ya vijana wenye umri wa miaka 17 ya Copa Coca-Cola, Mjini Magharibi wanatarajia kufungua pazia la michuano hiyo dhidi ya Kinondoni, katika mchezo utakaofanyika Ijumaa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.


Akizungumza Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Soka kwa Vijana, Msafiri Mgoi alisema kutokana na ratiba waliyoipanga, Mjini Magharibi inatarajia kufungua dimba dhidi ya Kinondoni.

Alisema mashindano hayo yanatarajiwa kushirikisha timu 28, kutoka Tanzania nzima, ambapo zimegawanywa katika makundi manne na kila kundi litakuwa na timu saba.

Mgoi alisema mashindano hayo yataanza, Ijumaa ambapo yanatarajiwa kufikia tamati Julai 10, mwaka huu na hatua ya awali itafanyikia Dar es Salaam na Pwani, kuanzia robo fainali yatahamia jijini Dar es Salaam.

Alisema hatua ya awali mashindano hayo, yatafanyikia katika viwanja vya Tamco, Nyumbu, Uhuru na Karume ambapo kila uwanja utakuwa na michezo miwili kila siku na robo fainali itafanyikia Uwanja wa Uhuru, ambapo kutakuwa na mchezo mmoja kila siku.

Mgoi alisema mashindano ya mwaka huu, yamefanyiwa marekebisho mbalimbali, ili kuweza kuyaboresha ikiwa ni pamoja na kuondoa lawama ambazo zimekuwa zikijitokeza mara kwa mara.

“Tumefanya marekebisho ya kutosha katika mashindano haya ya mwaka huu ikiwa ni pamoja na kuyaboresha zaidi, ambapo pia timu ambazo zinatoka sehemu moja, hazitaweza kukutana katika hatua ya awali,” alisema Mgoi.

Alisema Ijumaa katika Uwanja wa Karume, kutakuwa na mchezo kati ya Tabora na Pwani, Uwanja wa Nyumbu Pwani itakuwa ni Morogoro na Ilala, ambapo katika Uwanja wa Tamco kutakuwa na mchezo dhidi ya Kigoma na Temeke.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...