Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 16, 2010

MARCIO MAXIMO ATOA WOSIA KWA WATANZANIA


Maximo awapa wosia Watanzania

Na Shaban Mbegu

KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Marcio Maximo ambaye anamaliza mkataba wake mwezi ujao, amesema Tanzania inahitaji kuwekeza zaidi katika soka la vijana kuliko la wakubwa kama ilivyo hivi sasa nchini.

Akizungumza na Dar es Salaam jana, Maximo alisema kama kweli Tanzania inahitaji kupata maendeleo makubwa katika soka haina budi kuongeza mikakati kwenye soka la vijana ambalo ndiyo maendeleo ya mchezo huo katika miaka ya baadaye.

Alisema japokuwa watu wengi wamekuwa wakimbeza kutokana na timu ya taifa kushindwa kucheza michuano ya kiamataifa, tangu alipotua nchini, lakini anajivunia mambo mengi aliyofanya, hasa katika kuhakikisha mchezo huo unaanzia chini kwa vijana wadogo ambao ndio chimbuko la wachezaji wa baadaye.

Maximo alisema japokuwa muda wake wa kufanya kazi nchini umekwisha na tayari kocha mwingine wa kumrithi amepatikana, lakini kila siku atawashauri wadau wa soka wa hapa nchini kuwekeza zaidi katika vijana, kuliko kutegemea kupata mafanikio ya mapema kwenye timu ya wakubwa.

"Ili kuweza kuwa na timu nzuri itakayofanya vizuri katika mashindano ya kimataifa ni lazima ukubali kupoteza muda mrefu katika kuwaandaa vijana wadogo, ambao baada ya muda huja kuwa wachezaji wazuri wenye mafanikio kama watakavyokuja kuwa hawa vijana wa waliokwenda Afrika Kusini kushiriki Copa Coca-Cola", alisema.

Wakati huo huo Maximo, alisema wiki ijayo atawaaga Watanzania na kutoa tathimini yake juu ya soka la Tanzania kuanzia alipokuja nchini mpaka kufikia hivi sasa mkataba wake ulipofikia ukingoni.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...