Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 30, 2010

SOKO LA PAMOJA KUANZA KESHO

WAZIRI wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC),Dkt. Diodorus Kamala amewahakikishia watanzania kuondoa hofu ya kunyang'anywa ardhi yao kutokana na Tanzania kujiunga na Jumuiya hiyo.

Dkt.Kamala alisema kuwa ardhi ya Tanzania itabaki kuwa mali ya watanzania na haitaguswa na raia kutoka nje ya nchi kwa kisingizio soko la pamoja.

Hayo aliyasema Dar es Salaam juzi wakati akitoa ya utekelezaji wa majukumu ya wizara hiyo na kuongeza kuwa Tanzania inatazamiwa kunufaika na soko la watu milioni 130 kwa kuuza bidhaa zitokanazo na kilimo katika jumuiya baada ya kuboresha mazingira ya uzalishaji.

Dkt. Kamala alisema kuwa Tanzania ndio nchi pekee inayotarajiwa kutoa chakula kwa nchi za EAC kutokana na kuwa na ardhi nzuri ya mazao hivyo hatuna budi kutumia nafasi hiyo kuimarisha uchumi na maendeleo kwa ujumla.

"Jumuiya ya Afrika Mashariki imejaliwa kuwa na vyanzo vya maji, nishati, ardhi na hata mbolea hivyo kupitia jitihada za kikanda;Sekretarieti ya EAC imejipanga kuibua mpango wa kupatikana kwa utaratibu wa kuvuna mbolea itakayosaidia utekelezaji wa mkakati wa maendeleo ya kilimo,"alisema.

Aidha, Dkt. alisema kuwa suala la uuzwaji wa chakula nje ya nchi ambalo limekuwa kikwazo kwa wakulima kutokana na baadhi ya viongozi kuzuia limepitishwa na Mawaziri wa EAC na limewasilishwa kwa wakuu wa nchi hizo kutiliwa saini siku yoyote.

Alisema kuwa kitendo cha kumzuia mkulima kutouza chakula nje ni kumkwamishia maendeleo na malengo kwa kuwa ana uhuru wa kuuza nje kama nchi husika imeshindwa kununua kwa bei ya faida inayolingana na gharama alizotumia.

Vile vile alisema kuwa itifaki ya Umoja wa Forodha ya Afrika Mashariki mwaka 2004 imeridhiwa na nchi zote uanachama na malengo makuu ya itifaki hiyo ni kuondoa ushuru wa forodha kwa biashara ya bidhaa miongoni mwa nchi uanachama.

Pia kuweka wigo wa pamoja wa biashara wa ushuru wa forodha kwa bidhaa zitokazo nje ya jumuiya, kuweka vigezo vya jumuiya vya kutambua uasili wa bidhaa na kuondoa vikwazo visivyo vya kiforodha.

Dkt. Kamala alisema kuwa kila nchi kuorodhesha bidhaa nyeti zinazotozwa ushuru wa forodha kwa viwango vikubwa zaidi ya kiwango cha juu cha asilimia 25.

Alisema kuwa zipo bidhaa nyeti (sensitive Products) kutoka nje ya jumuiya ambazo hutozwa ushuru zaidi ya viwango hivyo vitatu ikiwa madhumuni ni kuzuia ushindani usio wa halina kulinda viwanda na uzalishani wa ndani. ya

Dkt. Kamala aliwataka watanzania kuwa wamoja wakati wa soko la pamoja kwa kusaidiana pale inapopatikana nafasi za ajira na kuachana na uoga ambao ni silaha ya udhaifu katika maendeleo.

Alisema kuwa watanzania wanatakiwa kuonesha uzalendo, nia, kujiamini na kudhubutu kupambana na soko la pamoja kwani wizara hiyo ipo sambamba katika kufanikisha elimu inawafikiwa wote kuhusu faida ya EAC na jinsi ya kukabiliana mabadiliko.

Hata hivyo alisema kuwa shirikisho hilo halitavunjika tena kama ilivyotokea mwaka 1977 kutokana na kutokana na mikataba madhubuti iliyowekwa ikiwemao ya sheria ya kila nchi yoyote iliyo EAC lazime ifuate sera za soko la uchumi na mengineyo.

Dkt. Kamala alisema kitendo cha nchi ya Kenya kupiga vita Tanzania kutouza pembe za ndovu kimetoa picha ya wazi kwa watanzania kutoa maamuzi ya kuridhia au la katika mazungumzo yanayoendelea sasa kuhusu suala hilo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...