Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 22, 2010

AJABU YA SOKA LA BONGO TIMU YA POLIS MBEYA YAENDA LINDI BILA DAKTARI WA TIMU


Na Moses Ng’wat,
Mbeya.

IKIWA imeanza maandalizi ya michuano ya ligi ya taifa ngazi ya makundi jijini hapa, timu ya Polisi Mkoa wa Mbeya, imebainika kufanya mazoezi bila kuwa na daktari wa timu hali ambayo ni hatari kwa afya za wachezaji.

Timu hiyo ambayo ilianza kambi tangu mei mwaka huu chini ya mwalimu wake Maka Mwalyisi, imepangwa katika kituo cha mkoani lindi ambapo michuano hiyo itaanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi huu.

Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima umebaini kuwa timu hiyo licha ya kutoandamwa na majeruhi katika kambi hiyo ya maandalizi haina daktari wa timu, jambo ambalo limekuwa likiwawweka katika wakati mgumu wachezaji.

Wachezaji waliozungumza na mwandishi wetu wamelalamikia kitendo hicho cha kutokuwa na daktari katika kambi yao na kueleza kuwa wameshindwa kuonyesha uwezo zaidi kutokana na kuwa na hofu ya kuumia na kukosa mtu wa kuwasaidia.

Kadhalika wadau wa mchezo huo na timu hiyo ya polisi wameponda tabia hiyo ya viongozi wa klabu hiyo kwa kushindwa kujali hali za wachezaji wake, ilhali wakijua fika kuwa timu hiyo inahitaji maandalizi makubwa kwa ajili ya mafanikio.

Walionyesha wasiwasi mkubwa juu ya majaaliwa ya mchezo huo mkoani hapa, wakidai kuwa maandalizi ya namna hiyo ni dhahiri kuwa maendeleo ya mchezo huo hayana maono ya mbali,huku wakikumbukia machungu ya kuporomoka kwa timu ya Prisons na kuuacha mkoa huo katika simanzi.

Kwa upande wao maofisa wa jeshi la polisi ambao wako na timu hiyo wakizungumza kwa masharti ya kutoandikwa majina yao, walishangazwa na uongozi kushindwa kujipanga kwa hilo.

Walisema ni ajabu kwa jeshi hilo lililosheheni watu wenye ujuzi wa hali ya juu katika kutoa huduma kwenye kada hiyo kushindwa kuandamana na timu hadi kuwepo na malalamiko.

“Hawako ‘siriazi viongozi wetu, huwezi kukusanya zaidi ya watu 20 halafu ukashindwa hata kuwa na huduma ya kwanza” alilalama mmoja wa maofisa hao.

Kwa mujibu wa mwalimu wa timu hiyo ya Polisi Maka Mwalyisi wanatarajia kuondoka juni 26 kuelekea mkoani Lindi huku akijinadi timu hiyo kuwa vizuri ukiondoa kasdoro hiyo ambayo alidai tayari imeshafikishwa kwa viongozi wa timu hiyo na kwamba inashughulikiwa.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...