Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, September 13, 2010

MASINDANO YA Safari LAGER POOL KUANZA SEPT 16 ARUSHA


Meneja wa bia ya Safari Lager,Fimbo Buttallah akitangaza rasmi tarehe ya kuanza kwa fainali za Taifa za mchezo wa Pool,zitakazifanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 16 mwezi huu.kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mchezo wa Pool Taifa (TAPA),Amos Kafwinga.na Mwenyekiti Aisac Togocho



Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager, ambao ni wadhamini wakuu wa mashindano ya Taifa ya Pool “Safari Lager National Pool Championship”, leo imetangaza rasmi tarehe ya kuanza kwa fainali za taifa za mchezo huo zitakazofanyika Matongee Club - jijini Arusha wiki hii.

Katika hatua ya kwanza iliyoanza tarehe 13 Julai na kukamilika mapema mwezi Agosti, timu zilishindana katika mfumo wa club katika mikoa 14 ya Tanzania bara na hatimaye kuunda timu za mikoa (combine) ambazo zitakutana katika jiji la Arusha kutafuta mshindi wa Taifa.

Katika fainali za mwaka huu, ambazo kwa mara ya kwanza zinafanyika katika kanda ya Kaskazini, zinatarajiwa kuwa za aina yake kufuatia maandalizi ya kutosha na maboresho makubwa yaliyofanyika katika uendeshaji wa fainali hizi.

Akizungumzia juu ya maandalizi hayo, meneja wa bia ya Safari lager Fimbo Butallah alisema; “maandalizi yote kwa ajili ya fainali yamekamilika na hivi sasa tunasubiri muda tu ili fainali zianze, tumejipanga inavyotakiwa katika pande zote na tunawaomba wakazi wa jiji la Arusha na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi katika ukumbi maarufu wa Matongee Club ulioko viwanja vya Nane nane – Njiro ili kuja kuzishangilia timu za mikoa yao na kujionea jinsi mchezo huu unavyochezwa katika viwango vya kimataifa..

Kuhusu suala la gharama kwa timu shiriki, Butallah alisema; Safari Lager inagharamikia kila kitu kuanzia nauli za kwenda Arusha na kurudi kwa mikoa yote shiriki, malazi, chakula na usafiri wa ndani wakati timu zitakapokuwa Arusha”.

Fainali hizo zinatarajiwa kuanza tarehe 16 Septemba na kufikia kilele tarehe 19 Septemba mwaka huu, mikoa itakayopambana katika fainali hizo ni pamoja na Ilala, Temeke, Kinondoni, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Manyara, Dodoma, Mwanza, Iringa, Mbeya, Shinyanga, Kagera na wenyeji Arusha..

Akizungumzia upande wa ufundi, Katibu mkuu wa chama cha Pool Taifa (TAPA), Amos Kafwinga alisema; “Tumejipanga vizuri sana katika kuhakikisha kuwa fainali hizi zinakuwa za aina yake na kuleta msisimko mkubwa na burudani ya kutosha kwa wapenzi na mashabiki wa mchezo huu jijini Arusha na maeneo ya jirani. Benchi la ufundi tayari limeshawasili jijini Arusha kuhakiki mambo yote yanayotakiwa ikiwa ni pamoja na meza zitakazotumika, hoteli za timu husika, usafri wa ndani wa timu, waamuzi nk.

Mshindi wa kwanza kwa upande wa timu mwaka huu atajinyakulia kitita cha shilingi 3,500,000/- pamoja na kikombe ,mshindi wa pili atapata shilingi 2,500,000/- na medali wakati mshindi wa tatu atajipatia shilingi 1,500,000/- na medali pia. Katika kipengele cha mchezaji mmoja mmoja (Singles) mwaka huu upande wa wanaume na wanawake ambapo mshindi upande wa wanaume atapata kitita cha shilingi 300,000/= na upande wa wanawake atapata 200,000/-.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...