Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, November 10, 2010

HAMISI MA SMS WA ZANTEL AIBUKA SOKO LA KARIAKOO NA KUWAFANYIA WATU SHOPING




KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zantel, imendelea na uwamasishaji wa Promosheni ya
'Hamisi Ma SMS'.

Akizungumza katika soko kuu la Kariakoo Dar es Salaam leo, Mtaalamu wa Bidhaa za Zantel, Bw.Deogratius Ringia alisema hadi kufikia jana jumla ya wateja
34 wameshinda zawadi za milioni moja.

Alisema wametembelea soko hilo kwa ajili ya kuitambulisha jamii kuwa wana uwezo mkubwa wa kushiliki na kushinda katika promosheni hiyo ambapo Bi. Diana Mwenga mkazi wa mwananyamala alibahatika kununuliwa vitu mbalimbali vya sokoni
.

Mbali na hivyo kupitia promosheni hiyo wamefanya kuwalipia nauli za daladala kwa abiria mbalimbali wa jijini wakazi waliobahatika kulipiwa nauli ni wakazi wa Mbagala na Mwenge.

"Nawapongeza wateja waliobahatika kushinda nawaomba wateja wetu waendelee kushiriki bahati nasibu hii ili waendelee kujishindia zawadi za kila siku na za mwezi," alisema.

Jinsi ya kushiriki promosheni hiyo unatuma neno HAMISI kwenda namba 15587 kwa gharama ya sh. 350 kwa kila ujumbe



No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...