Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, December 8, 2010

Madrid yajutia kumkataa David Silva






*Miaka 10 awa lulu

*Kuwatoka euro milioni 25



NI kawaida kwa klabu kubwa za Ulaya wakati wa usajili kuwafanyia majaribio wachezaji wengi, lakini siyo wote wanaopata nafasi ya kusajiliwa.



David Silva, ni mmoja wa washambuliaji walokutana na mkasa huo miaka 10 iliyopita, wakati huo akiwa katika kampeni yake ya kuimraisha na kung'arisha nyota yake katika soka la kulipwa.



Muda huo wa miaka 10 iliyopita, mshambuliaji huyo alifanya majaribio ya kutaka kuichezea klabu ya Real Madrid, lakini aliachwa kwa kile walichodai ni mfupi.



Uamuzi huo haukumvunja moyo mshambuliaji huyo, na badala yake aliendelea kufanya majaribio katika timu nyingine na kufanikiwa.



Valencia, wao hawakuwa na wasiwasi na kimo chake, walimpa karatasi na kuhitaji saini yake, matunda yake yanaonekana hivi sasa.



Pamoja na Madrid kumwona kuwa, hana uwiano na wachezaji wao, lakini kwa Valencia ilikuwa tofauti, kwani walimsaini na mpaka sasa amekuwa mpachika mabao mzuri katika Ligi ya Hispania 'La Liga'.



Maumivu yatakayowapata Real Madrid kumsajili mshambuliaji huyo kabla ya kwenda kwenye fainali za Kombe la Dunia Juni mwaka huu nchini Afrika Kusini, ni makubwa, watatakiwa kutoa euro milioni 25 kwa Valencia.



Rais wa Real Madrid, Florentino Perez, alisema kuwa, anahitaji kasi katika safu yao ya ushambuliaji, hivyo mawazo na akili yake yako kwa Silva.



Lengo lake ni kuhakikisha anapata saini yake haraka, mara baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu Hispania ama kabla ya kwenda kwenye fainali za Kombe la Dunia Juni mwaka huu.



Pia, Real Madrid wanajua fika kuwa, Manchester United, miamba mingine ya soka barani Ulaya, wanamtolea macho mshambuliaji huyo.



Hivyo, watakuwa na kazi kubwa na ya haraka kuhakikisha wanazima ndoto za Manchester United kumpeleka England katika Ligi Kuu ya huko.



Jina la familia yao ni Jimenez na jina la pili ni Silva.



David Josue Jimenez Silva, alizaliwa Januari 8, 1986 katika mji wa Arguineguin, Gran Canaria, katika kisiwa cha Canary, ni mchezaji wa kimataifa wa Hispania mwenye mchanganyiko wa asili ya Korea na Hispania.



Hivi sasa, mchezaji huyo anachezea klabu ya Silva, Valencia CF na timu ya taifa ya Hispania.



Silva ana uwezo wa kucheza pembeni ama namba 10, na wakati mwingine husaidia mashambulizi.



Ni mchezaji ambaye hufananishwa na Pablo Aimar uchezaji wake, alichukua nafasi ya mchezaji huyo katika klabu ya Valencia, pia huvaa jezi yenye namba 21, ambayo ilikuwa ikivaliwa na Aimar.



Silva alianza soka lake la kulipwa msimu wa 2004–05, katika ligi ya chini 'Segunda, akiichezea SD Eibar, akitokea Valencia CF kwa mkopo, alicheza mechi 35 na kufunga mabao matano.



Msimu uliofuata alikwenda kuitumikia Celta de Vigo kwa mkopo, huko alicheza mechi 34, alifunga mabao manne.



Silva alirejea Valencia msimu wa 2006, na kuwa chagua la kwanza pamoja na kuwa mdogo, wakati huo akiwa na miaka 20.



Katika misimu miwili, alikosa mechi sita wakati aliapchika wavuni mabao 14, bao la kwanza likiwa la Novemba 5, 2006 dhidi ya RCD Espanyol ambayo walifungana bao 1-1.



Baada ya kutoonekana miezi miwili ya msimu wa 2008–09 kutokana na maumivu ya kifundo cha mguu 'ankle', Silva alirejea uwanjani katikati ya Desemba.



Januari 3, 2009, alifunga mabao mawili katika mechi ambayo waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 nyumbani kwao dhidi ya Atletico de Madrid, na kuchangia mabao manne katika mechi 19 na kuisaidia kucheza michuano ya Europa.



Silva kwa mara ya kwanza kuiwakilisha Hispania sambamba na Cesc Fabregas ilikuwa mwaka 2003, katika mechi za Kombe la Dunia kwa Vijana wenye miaka chini ya 14 nchini Finland, alipachika wavuni mabao matatu.



Mwaka 2006, katika fainali za Kombe la Dunia kwa vijana wenye miaka chini ya 21, alifunga mabao mabao manne.



Katika fainali hizo, aliibuka mfungaji mabao wa nne katika michuano hiyo, akiwa na mshambuliaji wa Italia, Graziano Pelle.



Silva aliitwa katika kikosi cha kwanza kilichoichapa Romania bao 1-0, mechi hiyo ilikuwa ya kirafiki Novemba 15, 2006.



Aliendelea kuitwa katika timu ya taifa mara kwa mara kutokana na mchango wake mkubwa katika mechi yake ya kwanza.



Agosti 22, 2007, Silva aliifunga Hispania mabao mawili, katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ugiriki ambayo walitoka uwanja na ushindi wa mabao 3–2. Baadaye, aliitwa tena katika kikosi cha wachezaji 23, waliocheza fainali za UEFA 2008.



Katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Russia, Silva alifunga bao la tatu kwa kuunganisha pasi iliyotoka kwa Cesc Fabregas.



Katika mechi ya fainali, Silva alikumbana na matatizo baada ya kugongana na Mjerumani Lukas Podolski.



Kutokana na kugongana huko kulikomsababishia Podolski kwenda chini, kauli ya Mjerumani huyo kwa Silva haikuwa nzuri.



Matokeo yake, baada ya kutoleana maneno na kutunishiana misuli wakiwa kama wanatwanga vichwa, mwamuzi wa mchezo huo, hakuwaadhibu.



Muda mfupi, kocha wa Hispania wakati huo, Luis Aragones, aliamua kumtoa nje na nafasi yake ikachukuliwa na Santi Cazorla.



Mchezaji huyo mpaka sasa, anaichezea timu ya taifa ya Hispania na inawezekana akawa mmoja katika kikosi kitakachokwenda Afrika Kusini Juni mwaka huu kwenye fainali za Kombe la Dunia.



Hatua ya Real Madrid kumyantia mshambuliaji huyo, kutawafanya watoa fedha nyingi tofauti na wakati ule ambapo wangemtwaa kwa kitita cha chini.



Hivi sasa mchezaji huyo kutokana na kiwango alichokionesha, dau lake litakuwa kubwa.

1 comment:

  1. I'm gone to say to my little brother, that he should also visit this web site on regular basis to get updated from newest information.

    Feel free to surf to my web blog ... dominican

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...