Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, January 31, 2011

KAMPUNI YA TRUCKS YAKABIZI MALORI YA TAKA MANISPAA YA ILALA

Mkurugenzi wa Kampuni ya G.F Trucks & Equipment Ltd, Imran Karmal (kushoto) akimkabidhi mfano wa funguo, Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Slaa, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi malori sita ya kuzolea taka kila moja likiwa na thamani ya Sh. Milioni 115 kwa Manispaa hiyo, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo Barabara ya Nyerere Dar es Salaam leo mchana. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni hiyo, Mehboob Karmal. Wapili (kushoto) ni Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma ya Jamii na Uchumi, Angela Malembeka.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya G.F Trucks & Equipment Ltd, Mehboob Karmal (kulia) akimuonyesha Meya wa Manispaa ya Ilala, Jrry Slaa, Malori manne kati ya sita, yaliyotolewa na kampuni hiyo kwa Manispaa ya Ilala kwa ajili ya kuzolea takataka, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya magari hayo iliyofanyika kwenye ofisi za kampuni hiyo Barabara ya Nyerere Dar es Salaam.
Meya wa Ilala, Jerri Slaa, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
http://sufianimafoto.blogspot.com/

STANDARD CHARTERED WALA BATA NA WACHINA KUAZIMISHA MWAKA 2011 WAKICHINA


Baadhi ya wananchi wa Jamuhuri ya China wakichukuwa chakula cha usiku kilichoandaliwa na benki ya Standard Chartered wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya 2011 zilizofanyika Dar es Salaam, juzi. China waliadhimisha mwaka mpya kulingana na kalenda yao
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Muziki cha China, wakitumbuiza wakati wa maadhimisho ya sherehe za mwaka mpya 2011 zilizofanyika Dar es Salaam, juzi. China waliadhimisha mwaka mpya kulingana na kalenda yao

WAREMBO WANAOWANIA KISURA WA TANZANIA WAINGIA KAMBINI

WAREMBO wanaowania taji la Kisura wa Tanzania 2010/11, wameingia kambini leo katika Hoteli ya Kiromo View Resort, iliyopo nje kidogo ya Mji wa Bagamoyo,Pwani, tayari kwa fainali zitakazofanyika Machi 12, mwaka huu. Kambi hiyo itahusisha wasichana 25 kutoka mikoa mbalimbali nchini, waliofanikiwakutinga katika hatua ya fainali za shindano hilo, baada ya mchujo uliofanyika kwa miezi miwili.

Mchakato wa kuwapata wasichana
hao, ulianza Desemba 11, mwaka jana, na kumalizika mapema mwezi wa kwanza, ukihusisha warembo kutoka mikoa ya Mwanza,Mara, Kagera, Shinyanga, Tabora, Dar es Salaam, Arusha, Manyara, Dodoma, Iringa,Mbeya na Ruvuma.

Akizungumza wakati wa kuwatambulisha warembo hao katika Hoteli ya Kiromo ViewResort, Mwenyekiti na Mwanzilishi wa mradi wa Kisura wa Tanzania, Juliana Urio kutoka kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency (BTA), alisema kuwa warembo walioingia kambini, ni wale waliopita katika mchujo baada ya kukidhi vigezovinavyotakiwa.

Vigezo hivyo urefu wa sentimita174, mapaja 36, kiuno 25, kifua 36 na umri ni kati ya miaka 18-27, bila kujali kama mshiriki ameolewa, kuzaa au la.“Mwaka huu idadi ya warembo walioingia kambini imeongezeka, kutoka 20 kama ilivyokuwa awali hadi 25, hii ikitokana na mdhamini wetu Kiromo View Resort kutupa nafasi ya pekee ya kuongeza wasichana watano zaidi,” alisema.Urio aliwataja warembo walioingia kambini kuwa ni Neema Methew na Silipa Swai kutoka Mwanza, Lilian Bussa na Gaudencia Joseph (Mara), Beatrice James (Kagera),

Monica Fikiri na Angella Mombeki (Tabora).Wengine ni Suzana Manoko, Winnfrida Sabega, Rita Swai, Lethina Christoper, Joyce Joseph, Happiness Salimenya, Grace David (Dar es salaam), Dotinata Soro, Neema Kilango, Neema Seley (Arusha), Kipoyane Laibon (Manyara), Mariam-Kissa Isaack, Asha Hamisi, Flavian Makungwa, Lucy John (Dodoma) na Queen Kabisama (Ruvuma).

Alisema kuwa wakiwa kambini, warembo hao watapewa mafunzo mbalimbali kuhusiana na maisha yao binafsi na jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazowazunguka katika maisha yao ya kila siku, ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo tofauti. Urio aliwapongeza warembo waliopata bahati ya kutinga fainali za shindano hilo,ikiwa ni pamoja na kuwashukuru wazazi waliowaruhusu watoto wao kujiunga shindano hilo, akiwaahidi ‘kuwapika’ vilivyo warembo hao ili waweze kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii ya kitanzania kutokana na matendo yao.

Mdhamini mkuu wa shindano hilo ambalo linafanyika kwa mara ya tatu sasa, ni Family Health International (FHI), wakati wadhamini wengine ni TBC1, Kiromo View Resort, TanFoam (Arusha), SBC Limited, Flare Magazine, Hugo Domingo, BASATA, GRM Production, Clouds FM, ATCL na MJ Records.

CHANETA NA CHANEZA ZAKUTANA NA BMZ PAMOJA NA BMT

Mwenyekiti wa CHANETA ANNA BAYA wa kwanza kushoto akifuatiwa na makamu mwenyekiti SHY ROSE BHANJI pamoja na Katibu msaidizi ROSE MKISI.

Vyama vya netiboli TANZANIA BARA na VISIWANI vimekutanishwa na mabaraza ya michezo BARA na VISIWANI ili kumalizi migogoro katika vyama hivyo ambavyo vimekuwa katika mgogoro kwa muda mrefu.

Mkutano huo umewakutanisha wajumbe kutoka CHANEZA na CHANETA chini ya BMZ na BMT ambapo mwenyekiti wa baraza la michezo nchini IDD KIPINGU amesema sheria kali itachukuliwa iwapo vyama hivyo havitamaliza migogoro

Kutokana na migogoro katika vyama hivyo wanashindwa kushirikiana katika kuandaa timu ya TAIFA ya netiboli pindi inapohitajika kushiriki katika mashindano mbalimbali.

Mshindano ya ligi ya muungano yameshindwa kufanyika kutokana na migogoro ambayo inaendelea katika vyama hivyo.

Sunday, January 30, 2011

SHEIKH MKUU AWASILI GEITA KWA AJILI YA HARAMBEE YA UJENZI WA SHULE

Mkuuwa wilaya ya Geita Mh. Philemoni Shelutete, (kati) akimpokea Sheikh mkuu wa Tanzania Sheikh Issa Bin Shabani Simba, (shoto) katika ikulu ndogo ya Geita. Kulia ni Sheikh mkuu wa wilaya ya Geita Sheikh Haadi Kabaju. Mufti Simba, anatarajiwa kuongoza harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenziwa shule ya kiislamu wilayani humo leo.
Umati mkubwa wa waumini wa Dini ya kiislam, wa geita, wakishiriki maandamano maalum yalioandaliwa kwaajili ya kumpokea Sheikh mkuu wa Tanzania, Sheikh issa Bin Shabani Simba, aliyewasili jana mjini hapa, Sheikh Simba anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule ya kiislam ya Geita, harambee hiyo itafanyika leo hapa Geita.
http://issamichuzi.blogspot.com/

MWAKA MPYA WA KICHINA ULIVYO SHEREKEWA DAR ES SALAAM

Wanautamaduni wa China wakitumbuiza kwenye sherehe za Mwaka wa Kichina zinazoendelea hivi sasa katika bustani ya Mnazi Mmoja garden jijini Dar na kuhudhuriwa na mamia ya wachina na Watanzania na wageni waalikwa toka mataifa mbalimbali
Wachina wakisherehekea mwaka mpya wao leo

Baadhi ya mamia ya Wachina wanaoishi Tanzania wakirusha vishada katika kusherehekea Mwaka Mpya wa China jioni katika bustani ya Mnazi Mmoja garden jijini Dar
Vijana wa Kitanzania wakionesha ustadi wao katika Shaolin Kung Fu leo viwanja vya bustani ya Mnazi Mmoja garden katika kusherehekea Mwaka Mpya wa Kichina



Vijana wakionesha vipaji vyao katika Kung Fu leo
mdau aliyepata kusomea China akionesha ujuzi wake leo



Baadhi ya wachina katika sherehe hizo



http://issamichuzi.blogspot.com/

mambo ya versity nite at new club maisha

Msanii Redsun kutoka nchini Kenya akikamua katika usiku wa Versity Nite ndani ya New Club Maisha.
Beka a.k.a Masuspender akifanya vitu vyake.
Vijana wa kazi toka T.H.T,Barnaba,Beka na Amini wakikamua vilivyo katika usiku wa Versity Nite ndani ya New Club Maisha,jijini Dar.
Belle 9 nae hakua nyuma katika makamuzi hayo ya ukweli kabisa ya Versity Nite.
Ukumbi ulifurika kwa uwingi wa wadau waliohudhuria usiku huo.

NI MWAKA WA MJOMBA BAND 20011

Sabriba John na Ismail wa Mjomba Band wakikamua usiku huu ndani ya Mzalendo pub.
Baadhi ya waimbaji wa Mjomba Band,toka shoto ni Sabrina John,Filloo pamoja na Aneth Kushaba (aliekuwa mshiriki wa Tusker Project Fame 2010) wakifanya kamuzi la ukweli kabisa ndani ya Mzalendo Pub usiku huu.
Kamera man wa mtaakwa mtaa blog uzalendo umeingia mfukoni na kuanza kuyarudi magoma makali yaliyokuwa yakiachiwa na Mjomba Band usiku huu.
hapa sasa......
Mjomba Mrisho Mpoto akipiga stori mbili tatu na Mh. Zitto Kabwe aliefika katika kiwanja hicyo kumpiga tafu Mjomba Mrisho Mpoto ambaye anapiga hapo kila siku za Alhamisi akiwa na bendi yake nzima.

Friday, January 28, 2011

BREKING NEWWWZ MSONDO WAPATA PIGO LINGINE

Hamisi Maliki 'Super Maliki'
Mwananamziki Hamisi Maliki katikati waliokaa akiwa na wakongwe wa bendi hiyo enzi za uai wake mwanamziki huyo amefaliki Dunia Alfajili ya leo katika hospital ya Agrikani Malapa Dar es salaam

Mwanamziki wa bendi ya msondo ngoma Music ,Hamisi Maliki 'Super Maliki' picha ndogo amefaliki Dunia mwanamziki huyo aliyekuwa akiimba sauti ya kwanza amefaliki katika hospital ya Agrikan Malapa Dar es salaa alfajiri ya kuamkia leo akisumbuliwa na limonia mazishi yatafanyika kesho mwanamziki huyo aliyejiunga na kundi hilo mwanzoni mwa mwaka 2010 alikuwa akiimba nyimbo za sauti ya kwanza

MABONDIA JUMA FUNDI NA FRANCIS MIYAYUSHO KUONESHANA KAZI KESHO

Mratibu wa mchezo wa ngumi harifa jonsine katikati akiwanyosha mikono juu bondia juma fundi kulia na Francisi Miyayusho kushoto

WAZIRI WA FEDHA,UCHUMI ZANZIBAR ACHEZESHA DROO YA AIRTEL KWA AJILI YA WANAFUNZI KUPATIWA VITABU


Waziri wa Fedha, Uchumi na Maendeleo ya Mipango wa Zanzibar, Omar Yusuf Mzee (kushoto) akitazama kwa makini jinsi majina ya shule za sekondari 104 nchini yanavyopatikana kuweza kupokea msaada wa vitabu katika airtel. Katikati ni meneja wa Huduma za Jamii wa Airtel, Tunu Kavishe. Droo ya kupata shule 104 za sekondari imefanyika jana katika shule ya sekondari Haile Sellasie, Zanzibar.

Thursday, January 27, 2011

KUNA HAJA GANI YA KUTUMIA NGUVU KWA MUUZA MADAFU HUYU


Wagambo wa Manspaa ya Ilala wakiwa wamemkamata muuza madafu aliyekuwa akifanya biashara kinyume na taratibu barabara ya Msimbazi Dar es salaam leo kuna haja gani ya mfanyabiashara mmoja kukamatwa na wanamgambo sita


Wagambo wa Manspaa ya Ilala wakiwa wamemkamata muuza madafu aliyekuwa akifanya biashara kinyume na taratibu barabara ya Msimbazi Dar es salaam

AICC YAKABIZI MSAADA WA VITABU KWA WANAFUNZI ARUSHA


wanafunzi,
Baadhi ya wanafunzi wakifurahia vitabu vilivyotolewa na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC). AICC ilikabidhi msaada wa vitabu hivyo vyenye thamani ya shilingi 6.9 milioni shuleni hapo jana ili kupunguza tatizo la uhaba wa vitabu katika shule hiyo.

BIASHARA MITAANI


Wafanya biashara ya ndizi wakitafuta wateja makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi Dar es salaam jana

VODA COM YAZINDUA SIMU KWA AJILI YA WATU WENYE MATATIZO YA MACHO

Mkuu wa kitengo cha Mauzo wa Vodacom Tanzania Upendo Richard akionyesha simu maalum kwa waandishi wa habari ambayo kampuni hiyo imeizindua leo kwa ajili ya watu wenye matatizo ya kuona na kusikia Kushoto ni Meneja mawasiliano wa kampuni hiyo Nector Foya na kulia ni Msimamizi wa kitengo cha mauzo wa kampuni hiyo Mgope Kiwanga.
Msimamizi wa kitengo cha mauzo wa Vodacom Tanzania Mgope Kiwanga(kulia) akimkabidhi simu mwandishi wa habari wa gazeti la The African Sylvester Joseph aliyejishindia Bahati nasibu mara baada ya kampuni hiyo kuzindua simu maalum kwa ajili ya watu wenye matatizo ya kuona na kusikia.
Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Said Mtulya akionesha simu yake aliyojishindia katika bahati nasibu mara baada ya kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kuzindua simu hizo maalum kwa ajili ya watu wenye matatizo ya kuona na kusikia,anayeangalia kulia ni Mkuu wa kitengo cha Mauzo wa Vodacom Tanzania Upendo Richard.


Na Mwandishi Wetu
Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, kampuni ya simu ya mkononi ya Vodacom Tanzania imezindua simu maalum kwa ajili ya watu wenye matatizo ya kuona na wenye matatizo ya kusikia.

Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Nector Foya, alisema Jijini Dar es Salaam, simu hizo ni tofauti na nyingine kwa kuwa zitawawezesha wateja wao wenye matatizo ya kuona na kusikia kupata huduma ambazo hazipo katika simu za kawaida.

Alizitaja baadhi ya huduma hizo maalum zilizopo katika simu hiyo ni pamoja na maandishi makubwa katika Keypad zake, sauti kubwa katika spika zake na king'ora maalum nyuma ya simu kitakachowawezesha wateja wao kukibonyeza wakati wa dharura.

"Simu hizi za aina yake zitawawezesha wateja wetu wenye matatizo kama hayo kupata huduma ambazo hazipatikani katika simu nyingine za kawaida, natoa wito kwa watanzania wenye matatizo kama hayo kuzichangamkia simu hizi" Alisema.

Alizitaja aina hizo za simu kuwa ni S306 ZTE ambazo zitapatikana katika maduka mbalimbali maarufu kama Vodashop au kwa mawakala wa Vodacom waliopo nchi nzima.

"Tumeamua kuja na simu hizi baada ya kugundua kuwa kuna watanzania wengi wanapata matatizo na simu nyingi kutokana na maandishi madogo, sauti ndogo, na kadhalika. Lengo ni kuwasaidia na kuhakikisha ya kwamba wanaendelea kupata huduma za msingi kwa kutumia simu zao za mkononi bila vikwazo vyovyote vidogovidogo," Alisema.

Alisema kwamba simu hizo zinaweza kutumiwa hata na wasioona kwani ikibonyezwa herufi hutoa sauti inayo kujulisha umebonyeza herufi gani. Hivyo basi ni simu maalum kwa watu maalum katika jamii yetu.

Vodacom Tanzania imekuwa ya kwanza hapa nchini kubuni huduma mbalimbali kwani mbali na simu hiyo,Vodacom mapema mwaka jana ilizindua simu inayotumia mionzi ya jua ambayo imekuwa ikisaidia sana wananchi mbalimbali ambao wanapata matatizo ya miundo mbinu ya umeme.

Vodacom pia imewarahisishia mamillioni ya watanzania kupitia huduma ya Vodafone M-Pesa, huduma inayowawezesha wateja kutuma na kupokea fedha kupitia simu zao za mkononi.

Mbali na kutuma pesa kwa ndugu na marafiki wanao tumia mtandano wa Vodacom. Wateja wana watumia jamaa walio katika mitandao mingine hapa nchini.

Alimalizia kwa kusema, leo tuna furaha kuwawezesha wateja wetu kuchati bure kwenye mitandao ya Face Book, the grid na Vodamail. Vodacom Tanzania itaendelea kuboresha huduma zetu mara kwa mara kwa ajili ya wateja wake na wananchi kwa ujumla.

WAREMBO WA MISS UTALII WATEMBELEA MRADI WA CHUMVI

Mwongoza Watalii Makumbusho ya Kale, Katika Kanisa la Catholic Pwani, Justin Roman Lui, akifafanua jambo na kuwaonyesha namna chumvi inavyopakiwa kwenye mifuko washiriki wa Miss Utalii waliopembelea Mradi wa Chumvi wa Nunge,Bagamoyo Mkoani Pwani leo.
Baadhi ya Washiriki Miss Tourism wakiwekachumvi katika vifurushi, Nunge Bagamoyo Pwani,Wakati wa ziara ya Washiriki hao walipotembelea Mradi wa Chumvi wa Nunge,Bagamoyo Mkoani Pwani leo.
Picha ya Pamoja wa Warembo hao.


Warembo wa Tanapa-Miss Utalii Tanzania 2011, jana walitembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya Utalii ikiwa ni katika mchakato wa kujifunza masuala mbalimbali yanayohusian na Utalii wa Ndani wa Tanzania, katika mkoa wa Pwani Bagamoyo.

Katika matembezi hayo warembo waliweza kujifunza namna Uzalishwaji wa Chumvi unavyotengenezwa kutokana na mabwawa ya maji kutoka bahari ya Hindi(Maji chumvi).

Akizungumzia Mradi huo wa Chumvi, Meneja wa Mradi, Nicolaus Meliha, alisema kuwa Chumvi hiyo inatengenezwa kutokana na mabwawa yatokanayo na maji chumvi yanayopatikana kutoka bahari ya Hindi.

“kiujumla mradi wetu huu ndiyo unaozalisha chumvi nyingi hapa nchini pamoja na kwamba pia zipo sehemu zingine kama Mikoa ya Lindi na Zanziba, lakini hapa kwetu chumvi zaidi ya tani mia kwa wiki huku soko la ajira kwa wakazi wa mkoa wakiendelea kunufaika na mradi huu, ila kwenu washiriki wa shindano hili mkiwa kama mabarozi mnapaswa kuutangaza kama moja ya kivutio cha Utalii kutokana na kwamba upo maeneo ya kale ya kihistoria”alisema Meliha

Na kuongeza kwamba hadi chumvi inapatikana inatokana na kukaushwa kwa maji chumvi yatokanayo na maji ya bahari ya hindi, ikiwa ni baada ya kukaa eneo moja lisilorusu maji kutoka na pia inategemeana sana na jua ili maji kukauka ba baada ya hapo chumvi upatikana.

Fainali za mwaka huu zitarushwa moja kwa moja (live) na kituo bora kabisa cha runinga StarTV cha jijini Mwanza. Zitafanyika Februari 5, 2011 ambapo wasichana zaidi ya arobaini watakuwa wakimsaka mmoja anayestahili kuvikwa taji la umalkia wa taifa wa Utalii nchini ambaye pamoja na kuwa balozi wa kimataifa wa utalii wetu pia atapata mkataba wenye thamani ya shilingi milioni mia moja na hamsini.

Kambi ya warembo hawa iliyopo hoteli ya Kiromo View Resort, imekuwa gumzo kubwa la jiji la Dar sasa kutokana na ukweli kuwa, utulivu, umakini na madhari ya hoteli hii vimekuwa kielelezo tosha cha kufanya ushindani uwe mkubwa miongoni mwa washiriki ambapo pia watawania tuzo (awards) zingine zaidi ya ishirini na nane zitakazowawezesha kushiriki mashindano mengine ya kimataifa na kuwakilisha mikoa au maeneo yao vema.

Kauli mbiu ya mashindano ya Miss Utalii mwaka huu ni “Ewe Mtanzania tembelea na tangaza hifadhi za taifa, utalii ni maisha na utamaduni uhai” ambayo kimsingi ndicho kielelezo yakini cha shindano kikilenga kuhamasisha utalii wa ndani miongoni mwa Watanzania ambaio wengi wao hawajui kabisa maana vivutio vya kitalii na kitamaduni vilivyopo nchini.

Hoteli ya Kiromo ambako Shindano hili litafanyika ni ya kitalii na yenye hadhi ya nyota tatu na iko umbali wa kilometa kumi tu toka mjini Bagamoyo. Kadhalika, inatoa Huduma zote za kisasa kwa umakini na ustadi mkubwa.

Aidha, wadhamini wakuu wa shindano ni Kiromo View Resort na Sahara Media Group inayomiliki kituo cha runinga cha StarTV, Radio Free Africa, Kiss FM na gazeti la Msanii Afrika.
http://othmanmichuzi.blogspot.com/

AIRTEL YAWAKUMBUKA WANA HABARI


KAMPUNI ya Simu za mkononi ya Airtel imeandaa bonanza litakaloshirikisha vyombo mbalimbali vya Habari ambalo limepangwa kufanyika Februari 12 mwaka huu katika viwanja vya Posta na Simu Kijitonyama, Dar es Salaam.

Bonanza hilolinatarajiwa kushirikisha wanahabari zaidi ya 500 kutoka katika vyombo arobaini hapa nchini likihusisha michezo mbalimbli.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano alisema lengo la bonanza hilo ambalo wanalianda kila mwaka ni kuimarisha ushirikiano baina yao na vyombo vya Habari na kuendelezamahusiano.

"Ni kawaida katika kila mwisho au mwanzo wa mwaka kufanya tathimini ya jumla ya pale tulipo na wapi tunakwenda na pia tunakitumia kipindi hikikukaa na kufurahi pamoja na watu wenye majukumu tofauti miongoni mwao ni nyinyi wanahabari.," alisema Mkuu huyo.

Alisema michezo ambayo itachezwa katika bonanza hilo ni mpira wa miguu utakaohusisha timu zawatu saba kutoka kila upande, kukimbia kwa magunia, kuvuta kamba, kushindana kunywa soda, na mingine mingiambapo zawadi mbalimbali zikiwemo vikombe zitashindaniwa na vyombo hivyo na washiriki binafsi.

Beatrice alisema bonanza hilo mwaka huu limeboreshwa zaidi ya msimu uliyopita na kwamba kutakuwa burudani kutoka kwa bendi ya muziki waambayo itatangazwa baadae.

Hata hivyo alisema wataendelea kutoa taarifa za jinsi wanavyoendelea na taratibu za maandalizi ambapo pia wanakaribisha maoni kutoka katika vyombo vya habari kuelekea katika bonanza hilo.

Naye Mratibu wa Tamasha hilo na mwakirishi wa Kampuni ya Capital-Plus International ambao ndio waratibu, Mawazo Waziri alisema alisema maandalizi yanaendelea kufanyika kwa mafanikio makubwa na kuongeza kuwa kutakuwana mashindano ya kuimba na kucheza.

Tuesday, January 25, 2011

HASANI MOSH TX JR APAGAWISHA MASHABIKI MSONDO

Hassani Moshi JR akifanya makamuzi
Hassani Moshi JR akimba katika kundi la Msondo ngoma


Romani Mng'ande, Hassani Moshi JR na Eddo Sanga wakitoa burudani


Mwimbaji wa Bendi ya Msondo Hassani Moshi TX JR, kushoto akiimba wakati wa onyesho lao lililofanyika katika ukumbi wa Max baa Ilala Bungoni juzi, kulia ni mpiga gitaa Zahoro Bangwe

TAMASHA LA SAUTI ZA BUSARA LAZINDULIWA LEO


Mwimbaji wa muziki wa kizazi kimpya, Juma Kasimu 'Juma Nature' (kulia) akipeana mkono na Meneja Mkuu wa Zantel Zanzibar ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha la Sauti za Busara, Nahaat Mahfoudh wakati wa mkutano wa kutangaza Tamasha hilo, Dar es salaam jana katikati ni Makamu mwenyekiti wa Tamasha hilo, Simai Said

Mwimbaji wa muziki wa kizazi kimpya, Juma Kasimu 'Juma Nature' akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kutangaza Tamasha la Sauti za Busara, Dar es salaam jana litakalofanyika mwanzoni
Februari 9-13.Juma Nature ni kati ya wasanii watakaotumbuiza katika tamasha hilo, kushoto ni Meneja Mkuu wa Zantel Zanzibar ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha hilo, Nahaat Mahfoudh na Makamu mwenyekiti wa Tamasha hilo, Simai Said.

Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti za Busara,Yusuf Mahmoud akizungumza katika mkutano wa ufunguzi rasmi wa tamasha hilo kwa vyombo vya habari asubuhi hii katika hoteli ya Southen Sun,jijini Dar.katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Tamasha hilo,Simai Said na kulia ni Nahaat Mahfoudh kutoka Zantel.Meneja wa Tamasha la Sauti Za Busara,Stella Stephen akizungumza katika mkutano huo.wengine ni Mkurugenzi wa Masoko wa Zantel,Brian Karokola,Mkurugenzi wa Tamasha la Sauti Za Busara,Yusuf Mahmoud,Makamu Mwenyekiti wa Tamasha la Sauti za Busara,Simai Said na Nahaat Mahfoudh kutoka Zantel.
Baadhi ya Wanahabari na Wasanii walioshiriki katika mkutano huo.
Ankal akiwa na wadau wa Sauti Za Busara,toka shoto ni Yusuf Mahmoud,Waziri Ally, Nahaat Mahfoudh kutoka Zantel pamoja na Simai Said.

Sauti za Busara ni moja ya matamasha yenye mvuto wa kipekee barani Afrika, mwaka huu litafanyika kwa mara ya nane visiwani Zanzibar katika Mji Mkongwe kuanzia Februari 9-13.
Tamasha hili hukutanisha watu wa tamaduni mbalimbali na kuwaweka pamoja, wakisheherekea na kufahamiana kama alivyosema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete katika hotuba yake ya ufunguzi wa tamasha la mwaka 2010.

“tukio hili ni muhimu kwa kuwa linatoa fursa kwa wageni na wenyeji wa tamaduni mbalimbali kubadilishana mawazo,kuonyeshana upekee wao, utajiri na utofauti wa muziki wetu. Kwa ujumla linachangia kuimarisha muingiliano wa tamaduni na urafiki.”

Sauti za Busara huwakutanisha wasanii wakubwa wa muziki barani Afrika pamoja na kuibua vipaji vingine nchini. Mwaka huu vikundi 40 vitatumbuiza, baadhi ni, Orchestre Poly Rythmo de Cotonou (Benin), Blick Bassy (Cameroon), Otentikk Street Brothers (Mauritius), African Stars Band aka Twanga Pepeta (Tanzania), Mlimani Park Orchestra (Tanzania), Kwani Experience (South Africa), Culture Musical Club (Zanzibar), Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta ft. Bi Kidude (Zanzibar), Jagwa Music (Tanzania), Bismillahi Gargar (Kenya), Maulidi ya Homu ya Mtendeni (Zanzibar), Djeli Moussa Diawara (Guinea), Christine Salem (Reunion), Yaaba Funk (UK), Muthoni The Drummer Queen (Kenya), Jahazi Modern Taarab (Tanzania), Les Frères Sissoko (Senegal), Sukiafrica Sukiyaki Allstars (Pan Africa / Far East), Groove Lélé (Reunion), Vusa Mkhaya & Band (Zimbabwe / Various), Djaaka (Mozambique), Nomakanjani Arts (Zambia), Percussion Discussion Afrika (Uganda), Tunaweza Band (Tanzania), Staff Band Namasabo (Tanzania), Lelelele Africa (Kenya), Atemi & the Ma3 Band (Kenya), Sauda (Tanzania).

Sherehe za mwaka huu zitafunguliwa na maonyesho mbalimbali ya kuvutia, muziki wenye nakshi mbalimbali ikiwemo nyimbo za kiswahili, madansa, maonyesho ya vipande vya filamu za muziki kutoka Tanzania, Uganda, DRC, Ivory Coast na Senegal.

Wakati huohuo, tamasha litadhamini Busara Xtra, yaani matukio ya nje ya tamasha yatakayoandaliwa ndani ya Zanzibar na ambayo yatawavutia na kuwanufaisha wageni waalikwa.
Hii itatoa fursa kwa wasanii wa ndani kuonyesha kazi zao, kuwahamasisha wageni kuendelea kutazama maeneo mengine ya visiwa na kuongeza kipato kwa watu wengi.
Mwimbaji wa muziki wa kizazi kimpya, Juma Kasimu 'Juma Nature' (kulia) akipeana mkono na Meneja Mkuu wa Zantel Zanzibar ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha hilo, Nahaat Mahfoudh wakati wa mkutano wa kutangaza Tamasha hilo, Dar es salaam jana katikati ni Makamu mwenyekiti wa Tamasha hilo, Simai Said

Sunday, January 23, 2011

Super D kocha mwenye matarajio ya kuwafikisha vijana mbali katika ngumi


Awaomba wadau kushirikiana nae kuwasaidia vijana
MICHEZO hasa mchezo wa ngumi ni miongoni mwa michezo wenye msukumo mkubwa ukiwa umewapatia vijana nafasi ya kuwavutia katika jamii hasa katika kpindi hiki ambapo jamii zinajihusisha kwa karibu na michezo.

Ipo michezo katika jamii hasa hapa nchini ambayo imepokelewa kwa kiwango cha hali ya juu na mingine ikiwa bado haijapatiwa nafasi kubwa kama ambavyo inaonekana.

Mfano wa michezo ambayo imepta nafasi kubwa ya kupendwa na watu wengi hapa nchini ni mchezo wa mpira wa miguu, mchezo wa ngumi, na mchezo wa mchezo wa kikapu ingawa takwimu zinaoneshwa kuwa m,chezo wa kikapu ni wa pili kupendwa hapa nchini.

Ukiachilia mbali michezo hii ipo michezo mingine ambayo bado haijapewa nafasi kubwa katika maeneo mengi kwa mfano mchezo wa kriketi, gofu, mchezo wa meza, mpira wa mikono, tenisi na mingine mingi.

Wadau wengi wa michezo hapa nchini wamekuwa wakijihusisha karibu na michezo lakini wanashindwa kusonga mbele kutokana na msukumo wa jamii katika michezo kuwa mdogo inayopelekea kukosa wadau kudhamini michezo.

Kocha wa kujitegemea wa ngumi anayefundisha klabu ya Ashati ya Ilala Jijini Dar es Salaam Rajabu Mhamila 'Super D' ameanzisha programu maalumu ya kuwafundisha vijana anayoiendesha katika ufukwe wa bahari ya Hindi, sehemu ya Coco Beach.

Akizungumza na mwandishi wa makala hii hivi karibuni jijini Dar es Salaam Super D alisema alisema ameamua kuanzisha ili kutumia vizuri kipaji chake alichopewa na wengine waweze kufaidika nacho nao waweze kufaidika nacho.

"Nimeona vijana wengi hawana kazi wapo tu mitaani na wanavipaji sasa nafundishwa kwa kujitolea ili kuibua vipaji vyao na hatimaye waweze kutimiza malengo yao katika maisha.," alisema Super D kocha wa ambaye aliwahi kuchezea klabu ya zamani ya ngumi ya Simba Boxing Jijini Dar es Salaa.

Super D ambaye kitaaluma ni mwandishi wa Habari na mpiga picha wa Magazeti ya Majira, Spoti Starehe, Maisha, Dar Leo na Business Times yanayochapishwa na Kampuni ya Business Times ya Jijini Dar es Salaam anasema anaamini vijana wengi wanaweze kufika mbali kupitia mchezo huu kama wakiwezeshwa.

Anasema alianza programu yake ya ufukweni mapema mwezi Mei mwaka huu na kufanikiwa kupata vijana wachache lakini idadi yao hivi sasa imeongezeka hadi kufikia nane.

Kocha huyo anasema inawezekana pengine vijana wana vipaji katika ngumi lakini hawajui sehemu ya kupata mafunzo hivyo anawakaribisha vijana wengi kuhudhuri katika maeneo hayo kila siku za jumamosi na jumapili.
Anasema alianza programu yake ya ufukweni mapema mwezi Mei mwaka huu na kufanikiwa kupata vijana wachache lakini idadi yao hivi sasa imeongezeka hadi kufikia nane.

Kocha huyo anasema inawezekana pengine vijana wana vipaji katika ngumi lakini hawajui sehemu ya kupata mafunzo hivyo anawakaribisha vijana wengi kuhudhuri katika maeneo hayo kila siku za jumamosi na jumapili.
Anasema mabondia aliokuwa nao hadi hadi sasa wanafuatilia kwa makini mafunzo yake ambapo wengi wao wameonekana kuonesha nia na mapenzi ya dhati na mchezo huo.

"Sina shaka nao hata kidogo wanafanya vizuri na nawapongeza wanafuatlilia kwa makini na wananielewa viwango vyao vinazidi kubadilika kila kukicha wananipa moyo na nadhani watatimiza lengo.," anasema.

Akizungumzia mafanikio yake hadi amefanikiwa kuwa kocha Super D anasema alianza kujihusisha na mchezo wa ngumi mwaka 1984 na kujipatia uzoefu mkubwa baada ya kuchezea klabu mbalimbali za mchezo huo jijini Dar es Salaam.
Anasema klabu alizowahi kuchezea ni pamoja na klabu ya zamani ya Boxing iliyokuwa chini ya klabu ya soka ya Simba mwaka 1984, klabu ya reli iliyokuwa inamilikiwa na mamlaka ya reli kariakoo, pamoja na klabu ya Amana ya Ilala zote za Dar es Salaam.


Super D anasema akiwa bondia alipata nafasi ya kucheza na mabondia mbalimbali akiwemo Mbwana Matumla, Rashid Ally, Husein Pazzi, Alfred Ngaloma na bondia Roja Mtagwa ambaye ndiye bondia aliwewahi kumshinda kati ya hao ambaye kwa sasa anacheza ngumi nchini Marekani.
Alisema mabondia wengine aliowahi kucheza nao ni Oscar Manyuka, na Said Chaku ambaye kwa sasa ni mwamuzi wa mchezo huo katika mashindano mbalimbali yanayofanyika hapa nchini.
Hata hivyo hivi karibuni baada ya matunda ya kazi yake kuanza kuonekana kutokana na watu wengi kupendelea kupita na kutazama kazi yake baadhi ya wadau wameanza kujitokeza na kumpongeza.

Hata hivyo kocha huyo anasema anawaomba wadau wa mchezo huo wataungana naye kimsapoti ili kuwaendeleza vijana kutokana na ukosefu wa vifaa unaowakabili na wengi wao kushindwa kuhudhulia.

Anasema baada ya kuanza kazi yake hadi sasa amefanikiwa kumpata mdau mmoja aliyemtaja kwa jina la Zulfiqal Ali ambaye ameweza kumsapoti kwa kumpatia vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi laki tatu.

"Ninamshukuru sana na nina mpongeza kwa kitendo chake cha kiungwana kuniunga mkono kuwasaidia vijana, nafikiri mfano wake utaigwa na wadau wengine namhakikishia ataifurahia kazi yangu,." anasema kocha huyo.

Hata hivyo kocha huyo amewataka wadau wengine kumuunga mkono katika kazi yake ambapo pia amewaomba wazazi kuwaruhusu vijana wao ambao wanavipaji kuhudhulia mazoezi yake ili kuendeleza vipaji vyao.
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...