Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, January 20, 2011

Dr. Emmanuel Nchimbi akutana na Wamiliki wa vyombo vya habari

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga akimuonyesha jarida la Baraza Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo Dr. Emmanuel Nchimbi (kulia ). Wamiliki wa vyombo vya habari nchini (MOAT) na viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) walikuwa na mazungumzo ya kujadili mambo mbalimbali kuhusiana na taaluma ya habari na waziri Dr. Nchimbi leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo. Picha na Anna Nkinda - Maelezo

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (Maelezo) Raphael Hokororo, akifafanua jambo kuhusu sera ya habari wakati wa mazungumzo kati ya wamiliki wa vyombo vya habari nchini (MOAT), na viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo Dr. Emmanuel Nchimbi katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga.
Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari nchini Reginald Mengi (kulia) akizungumza jambo wakati wa mkutano huo leo. Kushoto ni Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo. Anayemsikiliza ni Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo Dr. Emmanuel Nchimbi .
Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo Dr. Emmanuel Nchimbi (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari nchini (MOAT) na viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao ulioganyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...