Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, April 6, 2011

ROLI LA MAFUTA LATUMIKA KUSAFIRISHA SHEHENA YA BANGI : POLISI WAWATIA NGUVUNI


Ni gari la kusafirisha mafuta aina ya Scania lenye namba za usajiri T263 BLL lililokamatwa na Jeshi la polisi mkoani Mwanza hii leo mara baada ya ukaguzi kufanyika na hatimaye kushikiliwa eneo la beria ya wilayani Magu mkoani Mwanza.

BANGI.
Awali katika ukaguzi huo kwenye beria ya Magu jeshi hilo liligundua shehena ya madawa ya kulevya hayo aina ya bangi kwa mzigo uliopakiwa juu ya tanki la mafuta ambao ulikamatwa na kupelekwa moja kwa moja kituo kikuu cha Polisi Mwanza.

"MURAaa RINGINE HIRI HAPA.!"
Lakini kituoni hapo wakati ushushaji ukiendelea, katika shughuli za upekuzi zaidi moja kati ya makachero wa jeshi la polisi aligundua shehena nyingine kubwa ya bangi iliyokuwa imehifadhiwa sehemu ya nyuma, chini ya tanki hilo la mafuta yenye upenyo mithili ya kisanduku cha kuhifadhia mizigo.

Ndipo ushushaji wa shehena hiyo ukafanyika huku ukiwapa shida washushaji kwani ilikuwa imeshindiliwa kiuakika mithili ya robota la pamba linavyshindiliwa.

DEREVA WA GARI HILO BASHIRI WAZIRI.
Inadaiwa kuwa Dereva wa gari hilo Bashiri Waziri alijaribu kudanganya kuwa ndiye aliyetoa taarifa kufanikisha muhusika wa shehena hiyo na zigo lake kukamatwa na jeshi hilo. Akisimulia kwamba eti' mara baada ya kupakia mzigo huo kutoka kwa mtuhumiwa asijue kama amebeba madawa haramu ya kulevya huku mmiliki wa mali hiyo akimwambia kuwa shehena hizo niza mbogamboga za majani anazosafirisha kuelekea jijini Dare s salaam, aliutilia mashaka baadaye njiani wakati wakipumzika kwenye baadhi ya vituo kwa kuhisi harufu kama ya bangi na ndipo alipo tafuta chemba na kuwapigia askari wa kituo cha beria kinachofata kuingia jijini Mwanza eneo la Magu ambapo askari walifanya upekuzi na hatimaye kubaini ukweli. MMMh!

MMILIKI WA ZIGO HILO MGESI ANTONY (41).
Katika tapatapa nae mtuhumiwa mmiliki wa zigo hilo haramu Mgesi Antony (41) kabila mkurya ambaye ni mkulima mkazi wa wilaya ya Tarime mkoani Mara alitamka dhahiri kwenye beria mahala alipokamatwa kuwa yuko tayari kutoa rushwa ya shilingi milioni moja kwa askari hao ili mzigo wake upate ruksa kuendelea na safari , askari hao waligoma na hatimaye kumfikisha kituo kikuu cha polisi Mwanza.
ZOEZI LA UPAKUAJI.

TBC AKIWAKILISHA.
Bangi hiyo ilikuwa ikisafirishwa kuelekea jijini Dar es salaam ilikuwa ikitoka eneo la Lamadi mkoani Mara eneo linalosadikika kuwa maarufu kwa biashara hiyo haramu tena wakazi wake wakichukulia poa’ yaani kama biashara nyingine za kawaida. Polisi inaendelea kuwashikilia watuhumiwa wote watatu akiwemo utingo wa roli hilo kwa ushahidi zaidi.

HABARI NA PICHA KWA HISANI YA http://uniqueentertz.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...