Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 22, 2011

HARAMBEE YA BARCLAYS KUSAIDIA AFYA YA MAMA WAJAWAZITO NA VICHANGA


Benki ya Barclays ya Tanzania, imetangaza kuanzisha mpango wake wa harambee unaoitwa Step Ahead. Kwa kusaidiana na Washirika wengine, Benki hii itaendesha zoezi la ukusanyaji wa fedha, kusaidia kutoa huduma ya afya kwa vichanga na mama wajawazito.

Hii Step Ahead ni ya pili kwa mpango huu unaosimamiwa na Benki ya Barclays Tanzania. Hatua ya kwanza ya mpango huu ilifanyika mwaka 2008, na michango yote ilikuwa kusaidia Taasisi ya saratani ya Ocean Road.

“Tumeweka lengo la makusudi, na tunategemea kukamilisha mengi zaidi mwaka huu,” amesema Afisa Mahusiano wa makao makuu ya Benki ya Barclays Tanzania, Kati Kerenge.

Fedha hizo zitakusanywa kupitia mpango mkakati wa ushirikiano na Mashirika mengine ambayo yataombwa kufadhili au kuchangia mpango huo kwa njia ya kuuza tiketi. Kilele cha tamasha hilo kitakuwa tarehe 10, ya mwezi Septemba mwaka huu wa 2011, wakati kutakapokuwa na matembezi ya kilometa 10 na kukimbia kilometa 5 ya Family Bazaar pamoja na tamasha la muziki, litakalowahusisha Wasanii wa ndani katika kuunga mkono tukio hilo.

Kadhalika mgeni rasmi wa siku hiyo ya Septemba 10, anatarajiwa kuwa mke wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mama Salma Kikwete. Aidha Benki hiyo imezialika Taasisi za Shirika la Umoja wa Mataifa (UNO), Serikali ya Tanzania, Taasisi binafsi na asasi za kiraia pam

oja na Washirika wao kusaidia mpango huo.

“Tuna bahati kwa kuwa tumepewa hamasa na mke wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano kwamba anaunga mkono mpango huu,” amesema mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Barclays Tanzania Bw. Kihara Maina. Na kuongeza “pia Barclays inajivunia kupata nafasi ya kuunganisha rasilimali watu na vifaa pamoja na jamii kusaidia mpango huu maalumu, ili kuweza kuleta mabadiliko kwenye jamii tunazozihudumia.”

Takwimu za vifo vya mama wajawazito Tanzania zinatisha. Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha kwamba wakina mama 35 wanakufa kila siku wakati wa kujifungua na zaidi ya 700 wanadhofika kiafya na kuathirika kutokana na ugumu wa kujifungua mtoto. Kuna kadirio la kesi zipatazo 3,000 za fistula Tanzania kila mwaka – hali ambayo haisikiki katika nchi zilizoendelea.

Takwimu za watoto wa umri chini ya miaka 5 zinaonyesha kuwa kiwango cha vifo hivyo ni kibaya, ambapo watoto 51,000 hufa kila mwaka katika mwezi wa kwanza wa maisha yao.

Benki ya Barclays imeunda mkakati

wa ushirikiano na taasisi ya CCBRT kuelezea suala hili kwa jamii ya Tanzania na inategemea kusaidiana na washirika wengine wa umma na binafsi kuhakikisha juhudi hizi chanya zinaleta matokeo chanya kwa nchi nzima.

“Tulikuwa na mwanzo mzuri kwa kuungwa mkono na mke wa Raisi na mashirika wengine na tunashukuru. Tunatoa pia shukrani zetu kwa DTP, ICAL, Movenpick, Delfina, Affinity PR, Raspak – kwa pamoja ambao wanaendelea kutoa michango ya mali kwa viwango visivyohesabika kufanikisha zoezi hili”, amesema Bi Kerenge. Kadhalika ameongeza kuwa “Barclays imeridhika kutoa mwongozo huu kwa washiriki wetu wenza, washirika na watu wa Tanzania kuja kwa pamoja kama jamii moja kuwasilisha mpango huu kikamilifu na kwa kueleweka.”

Kwa mtazamo wa kujenga uwezo wa wakunga, fistula, na upasuaji wenye tija kwa watoto waliozaliwa na kasoro zinazorekebika, Barclays inalenga kuifanya nchi kufikia viwango vya karibu vya 4 na 5 vya malengo yake ya afya MDG. Tanzania ni moja kati ya nchi 10 zinazochangia zaidi ya 60% ya vifo vya mama wajawazito na vichanga duniani.

“Sehemu ya malengo yetu makubwa ni kuweka tofauti ya kimaisha kwa watu wa tabaka la chini la wananchi” amesema Bw. Maina. Kwa kuhitimisha, ameongeza “Kwa Barclays, uraia unamaanisha kutekeleza wajibu wa mabadiliko katika jamii.”

Kwa kuongezea kwenye suala la watoto na afya ya mama wajawazito na waliojifungua karibuni, Benki ya Barclays imeshirikiana na Plan na Care International kuimarisha ubora wa maisha kwa watu maskini kwa kuongeza na kuendeleza fursa za huduma za kiuchumi; na pia kuhusu Junior Achievement (JA) kuhusu utayari wa mipango ya kazi kwa vijana.

http://fullshangwe.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...