Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 4, 2011

Lions Club Annual Masquerade Ball Kufanyika Jijini Dar es Salaam

Lions Club of Dar Host Frank Goyayi Addressing Media overlooking is Bongo Flava artiste Fareed Kubanda AKA fid Q and PR manager Exim Bank Linda Chiza.
Fareed Kubanda Lions club save your Sight Ambassaddor Stressing a point as Exim Banks Linda Chiza looks on.
Fashion designer jamilla Swai making a statement as Frank goyayi lions club of dar host president and Fid Q listening attentively.
----


· MAONYESHO YA KWANZA Tanzania YA Masquerade Ball
· Lions Clubs of Dar Host and Mzizima Kusaidia Jamii
· Wasanii kuungana kusaidia Jamii

Lions club annual annual masquerade ball itafanyika tarehe 11/ o6/ 2011 katika hoteli ya Kempiski kuanzia saa moja jioni. Hafla hii sio kwa ajili ya kuchangia kunusuru macho ya watanzania tu, bali pia hafla hii itakua ni tukio la kuwaleta pamoja viongozi wote wa Tanzania katika ngazi mbali mbali chini ya mwamvuli mmoja kwa nia moja ya kutumikia jamii inayowazunguka kwa kuchangia kunusuru uwezo wao wa kuona.

“Hii ni kwa mara ya kwanza kabisa kwa club hizi mbili Lions club of Dar Host na Mzizima kuungana nguvu kufanya hafla ya kuchangiza fedha kwa ajili ya wahitaji chini ya programu ya macho kwanza, kwa ajili ya watu wenye matatizo ya macho lakini hawana uwezo wa kupata huduma hii” alisema Frank Goyayi rais wa Lions club Dar Host ya jijini Dar es Salaam.

Tukisimama kwa pamoja na tukifuata nyayo na motto ya Lions Club “kutumikia jamii”, wasanii katika Nyanja tofauti wamejitoa kushiriki katika jambo hili. Wasanii hawa waliojitolea kwa hali na mali ni Fareed Kubanda (Fid Q), mchekeshaji Steve Nyerere, wabunifu wa mavazi Jamilla Vere Swai na Mustafa Hassanali.

“Kama kioo cha jamii na mmoja kati ya wasanii wanaongoza katika tasnia ya mziki wa Hip Hop, najisikia mwenye furaha na mnyenyekevu kutoa muda msaada wangu wa hali na mali kukuunga mkono kampeni hii na kama balozi wa Lions club natarajia kutoa msaada wangu wa hali na mali kuitumikia jamii ya wahitaji Tanzania” alisema Fid Q

Hafla hii ya kipekee kabisa kuwahi kufanyika nchini Tanzania itajumuisha, onyesho la mavazi, burudani mbalimbali, bendi, chakula cha jioni na muziki. Wageni wote wakao hudhuria katika hafla hii pia wanakumbushwa kuja na “mask” inaweza kuwa ya asili ya kiafrika au ya kimagharibi.

“Tunawashukuru wote waliotuunga mkono, kutudhamini na kusaidia kufanikisha tukio hili, tunatarajia kuchangisha fedha zitakazowezesha kufanyika kwa kazi hii kwa mwaka huu na pia tunatarijia kupata ushirikiano kutoka kwa jamii kufanikisha programu hii ya kusaidia macho ya Lions Club”. Alisema Mustafa Kudrati Secretari wa Lions club Mzizima

“Fashion 4 Vision Annual Masquerade Ball” limedhaminiwa na Exim Bank, kwa kushirikiana na Club Billicanas, Coca cola, Global Outdoor Systems, 2M Media, Lotus Creative Concepts, Choice Fm , Clouds TV, Fashion 4 Health, Daily news, Habari Leo, Oman Air na 361 Degrees.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...