Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, August 21, 2011

MWONGOZO WA KATIBA MPYA KWA RAIA HUU HAPA


Stewart Moshi na Servi Roman

MAELEZO

UONGOZI wa Jukwaa la Katiba Tanzania umezindua Mwongozo wa Katiba kwa Raia ili wananchi waweze kujadili na kutoa maoni yatakayowezesha utungwaji wa katiba mpya.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Bw.Deus Kibamba amesema wameandaa Mwongozo wa Katiba ili kuhakikisha mambo yanayopaswa kuzingatiwa katika katiba mpya ya Kidemokrasia yanakuwepo.

Bw.Kibamba amesema mwongozo huo utapatikana bure kwa lugha ya Kiswahili na kwa kila Mwananchi ili kila Mtanzania anayejua kusoma aweze kuielewa na kuchangia mawazo katika uundwaji wa katiba mpya.

Ameelezea kuwa mwongozo uliozinduliwa ni mahsusi katika kuelezea kwa ufundi taratibu na masuala muhimu ya kuzingatia katika mchakato wa kuandika katiba ya kidemokrasia hapa nchini kwetu.

“Mwongozo huo unatoa majibu ya maswali mengi wanayojiuliza Watanzania juu ya mchakato wa Katiba,umeelezea a kwa ufundi na wepesi utaratibu, mchakato wa masuala muhimu ya kuzingatia katika mchakato wa kuandika katiba ya kidemokrasia hapa nchini kwetu”.alisema Bw.Kibamba.

Aidha amesema Mwongozo huo umeangalia historia ya katiba ya sasa ,ikiwemo mabadiliko ya katiba yaliyopita yaliyosukuma upatikanaji wa katiba zote tano za nchi tangu uhuru (Tanganyika na Zanzibar ).

Mwenyekiti huyo amesema mwongozo uliozinduliwa utapatikana kila mkoa bara na visiwani kupitia vituo vya Jukwaa la Katiba Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...