Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, September 13, 2011

ADB YAIPA TANZANIA BILIONI 133 KWA AJILI YA ELIMU


Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo(kushoto) akibadilishana hati ya msaada wa kiasi cha bilioni 133 na Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) Tonia Kandiero(kulia) (leo) mjini Dar es salaam kwa ajili ya miradi ya kilimo na elimu nchini.

Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo(katikati) akijibu maswali ya waandishi wa habari (leo) mjini Dar es salaam mara baada ya kupokea hati ya msaada wa kiasi cha bilioni 133 kutoka kwa Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB) Tonia Kandiero(kulia) kwa ajili ya miradi ya kilimo na elimu nchini.

Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es salaam

(Na Esther Muze na Bebi Kapenya – MAELEZO)

Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa shilingi bilioni 133 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kusaidia miradi kuendeleza sekta ya kilimo na elimu nchini.

Msaada huo ulisainiwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa fedha Mustafa Mkulo kwa niaba ya Tanzania na Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Tonia Kandiero.

Akiongea mara baada ya kupokea msaada huo, Waziri wa Fedha alisema kuwa, fedha hizo zitasidia katika kuboresha sekta ya kilimo ikiwemo miundombinu ya masoko .

Aliongeza kuwa, sehemu nyingine ya fedha hizo itasaidia kutoa mafunzo kwa vijana wenye mahitaji maalum ambao walioacha masomo kabla ya kumaliza elimu yao kwa sababu mbalimbali.

Mkulo aliahidi kuwa Serikali ya Tanzania itahakisha kuwa msaada huo unatumika katika maeneo waliyokubaliana ili kuleta maendeleo kwa kwa wananchi na kupunguzia umaskini.

Naye Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Tonia alisema kuwa, msaada uliotolewa na Benki hiyo utasaidia Tanzania kiuchumi katika harakatio zake za kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

Aliongeza kuwa msaada huo utawasaidia vijana kupata ujuzi katika visiwa vya Zanzibar ambao watasaidia kuongeza nguvukazi katika soko la ajira kwa ajili ya kuleta maendeleo yao na nchi kwa ujumla.

Aidha alisema kuwa Benki hiyo itaendelea kuisaidia Tanzania ili kukuza maendeleo yake ya kiuchumi na kijamii.

Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa miaka mitatu iliyopita imekuwa ikitoa misaada ya kifedha kwa lengo la kuisaidia Tanzania kiuchumi.

http://fullshangwe.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...