Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, November 7, 2011

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI BARAZA LA IDD NA SWALA YA ID KITAIFA MSIKITI WA AL FAROUK DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake ya Baraza la Eid El-Haj, baada ya swala ya Idd iliyofanyikaKitaifa kwenye Msikiti wa Al farouq Kinondoni jijiji Dar es Salaam .
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wa kwanza (kulia) akishiriki Swala ya Idd El Haj, iliyoswaliwa katika Msikiti wa Al Farouk uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam leo. Mbele ni Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Muhidin Mkoyogole, akiswalisha swala hiyo iliyofanyika Kitaifa katika msikiti huo sambamba Baraza la Idd.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal Wa pili (kulia) Rais Mstaafu wa Comoro, Mohammad Abdallah Sambi (kulia) Kaimu Mufti Mkuu wa Tanzania, Ally Muhidin Mkoyogole na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, wakijumuika na waumini wa dini ya kiislam katika swala ya Eid El Haj, iliyofanyika Kitaifa katika msikiti huo sambamba na Baraza la Idd.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, wakati akipokelewa alipowasili katika viwanja vya Msikiti wa Al Farouk, Kinondo ni jijini Dar es Salaam leo, kushiriki katika swala ya Idd El Haj iliyofanyika Kitaifa katika msikiti huo sambamba na Baraza la Idd.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, akipokelewa na mmoja wa waumini wa dini ya Kiislam, Asha Baraka, wakati alipowasili kwenye viwanja vya Msikiti wa Al Farouk, Kinondo ni jijini Dar es Salaam kushiriki katika swala ya Idd El Haj.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwilima, wakati akiagana na wageni wake waliomtembelea kwenye makazi yake Oysterbay

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...