Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, November 11, 2011

VIONGOZI WA VILABU WAKUBALIANA KUTOHUDHURIA MKUTANO WA TENGA KESHO


Masaa machache baada ya Raisi wa shirikisho la soka nchini TFF, Leodgar Tenga kuomba kukutana na viongozi wakuu wa vilabu 14 vinavyoshiriki katika ligi kuu ya Tanzania bara kwa ajili kuzungumzia utata wa namna ya uendeshaji wa ligi kuu ya msimu ujao utakavyokuwa, sasa taarifa za muda huu zilizothibitishwa zinasema viongozi hao wa vilabu wamekutana jioni katika hoteli ya Movenpick na kuamua kuwa hawatokwenda kukutana na Tenga kesho kama alivyoomba.

Viongozi hao wa vilabu wamesema sababu kuu ya kukataa kwenda kufanya mazungumzo na Tenga ni kwa sababu hawadhani kwamba kuna jipya lolote wataloambiwa ili kuweza kubadili msimamo wao wa ligi ya msimu ujao kuendeshwa na kampuni ya vilabu.


“Hatuoni kama kuna umuhimu wowote wa kufanya majadiliano juu ya suala hili, sisi sote tumeshaamua kwamba msimu ujao ligi itaendeshwa na kampuni ya vilabu vishiriki, TFF na Tenga wenyewe hawataki, wanataka kamati itakayoteuliwa na Tenga ndio iendeshe ligi. Tenga anataka tukae tujadili ajenda ipi? Sisi kwa pamoja tumeshaamua kwamba ligi ya msimu ujao itaendeshwa na kampuni yetu na huu uamuzi wetu wa mwisho,” alizungumza Geoffrey Nyange Kaburu ambaye ni mwenyekiti wa Kamati maalum ya kusimamia mchakato wa uanzishwaji wa Kampuni ya kusimamia ligi kuu kuanzia msimu ujao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...