Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, January 12, 2012

BAADA YA KUUTEMA UBINGWA WA DUNIA KALAMA KUPAMBANA NA CHEKA JANUAR 28


BONDIA Karama Nyilawila ameibuka na kudai kitendo cha kunyang'anywa mkanda wake wa ubingwa wa Dunia wa WBF, na waandaaji wa mashindano hayo hakimsumbui kwani yeye anachoa angalia ni pesa.

WBF jana ilitangaza kumnyang'anya ubingwa huo kupitia kwa wasimamizi wa pambano hilo hapa nchini Rais wa Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania (PST) Emmanuel Mlundwa baada ya kutangaza kucheza pambano lisilo la ubingwa na Francis Cheka kitu ambacho hakitakiwi na WBF.

Akizungumza Dar es Salaam leo, Nyilawila alisema, hawezi kucheza pambano kwa kutafuta sifa bila kuwa na fedha kwani yeye anachoangalia zaidi ni maslahi.

"Kunyang'anywa ubingwa hakunitishi kama historia ya kuwa bingwa wa Dunia wa WBF mwaka juzi itabaki kuwa pale pale ingawa wameninyang'anya mkanda bila kupigwa, mimi natafuta pesa sifa hazina nafasi kwangu kwani ubingwa wa Dunia naweza kuwania hata katika mikanda mingene," alisema Nyilawila.

Alisema, amekaa kipindi kirefu bila kuwa na pesa na hata kupanda ulingoni sasa ameapata sehemu ya kujikwamua hawezi kuipoteza kwani hata pesa ambazo angezipata huko ni ndogo kuliko anazozipata katika pambano lake hilo na Cheka.

Alisema, kwa sasa ameishapandisha uzito hadi kg 75 ambao amesaini kucheza na Cheka sasa ingemuia vigumu kushush haraka uzito huo hadi kufikia kg 72 ambao alisaini katika ubingwa huo wa Dunia.

Aliongeza kuwa pambano lake na Cheka liko palepale na kwa sasa anaendelea kujifua na anaimani kumchapa hata wakifika raundi ya mwisho.

Naye kwa upande wake Promota wa pambano hilo Philemon Kyando alisema, maandalizi yanaendelea ambapo mabondia wote wapoa katika hari ya kushindana ambapo litasimamiwa na TPBC.

Aliwataja mabondia watakaosindikiza pambano hilo kuwa ni Maneno Osward 'Mtambo wa gongo' akicheza na Nasib Ismail, Chaulembo Palasa na Seba Temba, Venance Mponji na Ibrahim Elask na Antony Mathias akiwa na Juma Afande.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...