Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, February 25, 2012

RASHIDI MATUMLA VS MANENO OSWARD KUPAMBANA TENA LEO FEBRUARY 25 UKUMBI WA PTA SABASABA DAR...!!!







MAANDALIZI ya pambano lisilo la ubingwa kati ya mabondia Rashid
Matumla ‘Snake Man’ na Maneno Oswald ‘Mtambo wa Gongo’ lililopangwa
kuwa Februar 25 mwaka huu leo yanaenda vizuri.Promota wa mpambano huo Issa
Malanga, alisema pambano hilo limeandaliwa ili kumaliza ubishi baina
ya mabondia hao, ambao pambano la mwisho walitoka sare ya point 99.99

Hata hivyo Oswald aliwalalamikia majaji kuwa hawakumtendea haki.
Mabondia hao wamewahi kupambana mara nne, Oswald akishinda mara moja
na Matumla mara mbili na kutoka sare mara moja.

Alisema pambano hilo linatarajia kuwa la raundi 10 uzito wa kati,
litafanyika kwenye ukumbi wa PTA sabasaba Dar es salaam


Mpambano huo wa kumaliza ubishi baada ya kila mmoja wao kudai
alishinda katika mpambano wao wa mwisho

Aidha aliwataja wakali watakaosindikiza mpambano huo ni Shomali
Mirundi na Mikidadi Abdallah 'Tatson', na Iddy Mkenye atapambana na
Shabani Mtengela ' Zunga Boy', Abdallah Mohamedi na Saleh Mkalekwa
mbali na hayo mpambano mwingine ni Ramadhani Mashudu na Hassani Kiwale
'Moro Best

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye
mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Roy Jonas,Evander holyfield,Lenox Lewis, Manny Paquaio, Floyd Maywherth,
Roy Jones na wengine kibao ‘DVD’ hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali
ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha Rajabu Mhamila
‘Super ‘D’.
“Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika
pambano la Cheka na Maugo ili kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni
pamoja na sheria za mchezo wa ngumi,” alisema Super ‘D’

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...