Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, March 26, 2012

WATATU WAPATIKANA KUSHIRIKI MAONYESHO YA WIKI YA MKITINDO YA AFRIKA YA KUSINI


Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Millen happiness Magese (katikati) akipiga picha ya pamoja na washindi watatu waliopata tiketi ya kuonyesha mavazi katika wiki ya mitindo ya Afrika Kusini, Victor Casmir, Victoria Casmir na Anastazia Gura. Wengine katika picha ni Aminat Ayinde kutoka kampuni ya America Next top model cycle 12 (wa kwanza kushoto), Ritha Poulsen (wa kwanza kulia) na Mustapha Hassanali aliyesimama nyuma. Picha kwa hisani ya Millen Magese group of company
**************************************
Na Mwandishi Wetu, Jijini
Wanamitindo watatu, Anastazia Gura (21) na mapacha, Victoria Casmir (20) na Victor Casmir wameshinda usaili uliondeshwa na kampuni ya Millen Magese Group Company Limited chini ya mpango wake wa kuitangaza Tanzania kupitia fani ya mitindo ujulikanao kwa jina la Tanzania International Fashion Exposé (TIFEX).

Wanamitindo hao wamefanikiwa kupita katika usaili huo ambao uliwajumuisha wanamitindo 350 kutoka katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam na mikoa ya jirani.

Kutokana na ushindi huo, wanamitindo hao wanatarajia kuondoka mwishoni mwa mwezi huu kuelekea nchini Afrika Kusini kushiriki kwa mara ya kwanza katika historia katika fani ya mitindo ya wiki ya mitindo ya Afrika Kusini maarufu kwa jina la South Africa Fashion Week.

Akizungumza baada ya usaili huo, Millen alisema kuwa amestushwa sana na ujio wa wanamitindo mbali mbali mbali waliofika katika usaili huo japo alitangaza kwa muda mfupi.

Millen alisema kuwa awali alipanga kuchukua wanamitindo wawili, lakini kutokana na idadi kubwa iliyojitokeza, ameongeza nafasi moja kama shukrani yake ya witikio huo mkubwa.

Alisema kuwa walipata kazi kubwa sana kuchagua wanamitindo hao watatu, lakini kwa kushirikiana na wanamitindo maarufu Aminat Ayinde kutoka kampuni ya America Next top model cycle 12 na Ritha Poulsen, waliweza kufanikisha zoezi hilo mapema zaidi.

Millen alisema kuwa washindi hao wamepata fursa pekee ya kujitangaza wenyewe kimataifa na kufuata nyayo zake.

Alisema kuwa lengo kubwa la kampuni yake ni kuendeleza fani ya uanamitindo na vile vile kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake kwa kupitia fani ya mitindo na hata kwa njia ya utalii.

Aliongeza kuwa japo Tanzania ina wanamitindo wengi na wabunifu, bado kuna pengo kubwa ukilinganisha na maendeleo ya fani hiyo katika nchi ya Afrika Kusini na Nigeria.

Alisema kuwa nchi hizo zimepiga hatua kubwa sana na yeye kuhamasika kuanzisha kampuni yake iliyozinduliwa mwezi Machi mwaka jana kwa lengo la kuziba pengo hilo na kuleta maendeleo ili wahusika wafaidike na matunda ya fani yao.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...