Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, June 16, 2012

EDDA MISS KIGAMBONI CITY 2012



Redds Miss Kigamboni City  2012 , Edda Sylvester (21) akipunga mono kwa furaha mara baada ya kutangazwa mshindi na kuvikwa taji la Kigamboni City katika shindano lililofanyika katika Ukumbi wa Navy Kigamboni jijini Dar es Salaam jana. (Picha zote na Mroki Mroki) 
Warembo walioingia hatua ya tano bora ya Miss Kigamboni 2012, kutoka kulia Elizabeth Boniface, Ester Albert, Edna Sylvester, Hadija Kombo na Agnes Goodluck wakipozi kwa picha jukwaani baada ya kutajwa kuvuka nafasi hiyo na kupata tiketi ya kushiriki shindano la Miss Temeke 2012 baadea mwaka huu.
Warembo waliokuwa wakiwania taji la Miss Kigamboni City 2012 wakicheza show ya ufunguzi jukwaani.
Redds Miss Kigamboni City  2012 , Edda Sylvester (katikati) akiwa na mshindi wa pili Agnes Goodluck (kushoto) na mshindi wa tatu Elizabeth Boniphace mara baada ya kutangwazwa washindi. Edda aliwashinda warembo wengine 9 katika shindano hilo. (Picha zote na Mroki Mroki) 

Na Mwandishi Wetu
MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Mlimani jijini Dar es Salaam, Edda Silyvester, 21, usiku wa kuamkia juzi alifanikiwa kutangazwa kuwa mshindi wa taji la kitongoji cha Kigamboni 'Redd's Miss Kigamboni 2012' katika shindano lililofanyika kwenye ukumbi wa Navy Beach.
Kutokana na ushindi huo Edda alizawadiwa kitita cha Sh. 500,000 taslimu na mgeni rasmi katika shindano hilo, diwani wa Kata ya Kigamboni, Dotto Msawa.
Nafasi ya pili katika shindano hilo lililopambwa na burudani safi kutoka katika bendi ya FM Academia maarufu Wazee wa Ngwasuma ilichukuliwa na Agnes Goodluck ambaye naye alipata zawadi ya Sh. 350,000.
Elizabeth Boniface alichaguliwa kuwa mshindi wa tatu na kupata zawadi ya Sh. 300,000 huku nafasi ya nne ikienda kwa Esther Albert na mshindi watano akiwa ni Khadija Kombo. Elizabeth na Khadija kila mmoja alipata zawadi ya Sh. 200,000.
Jaji Mkuu wa shindano hilo, Benny Kisaka, alitangaza kuwa badala ya warembo watatu atachukua warembo wote watano kwenda kushiriki katika shindano la Kanda ya Temeke baadaye mwaka huu.
Warembo wengine walioshiriki shindano hilo walikuwa ni Sophia Martin, Rosemary Peter, Doreen Kweka na Linnah David waliambulia kitita cha Sh. 150,000 kila mmoja.
Waratibu wa shindano hilo, kampuni ya K& L Media Solutions wanawashukuru wadau wote waliosaidia kufanikisha shindano hilo
Kwa kufanikisha onyesho hilo ambalo lilikuwa ni la mwisho kwenye kanda ya Temeke.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...