Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 19, 2012

KINONDONI YATWAA UBINGWA DARTS MASHINDANO YA ´VISHALE´



Mwakilishi wa Mauzo wa TBL, Kanda ya Kinondoni, Endrew Misama (kushoto) akiwakabidhi Kombe la Ubingwa wa mchezo wa Darts Mkoa wa Dar es Salaam, wachezaji wa timu ya Kinondoni, baada ya kutwaa ubingwa katika mashindano ya ´Vishale´.



TIMU ya Kinondoni ya wanaume imefanikiwa kutetea ubingwa wa mashindano
ya Darts 'Vishale' Mkoa wa Dar es Salaam yaliyofanyika juzi, kwenye
Ukumbi wa Moshi jijini.

Mashindano hayo yaliyojulikana kama 'Dar es Salaam Darts Association
Tournament 2012', yalidhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL),
kupitia kinywaji chake cha Safari Lager.

Kinondoni imechukua ubingwa wa mashindano hayo kwa mara ya pili
mfululizo baada ya kuzishinda timu za Ilala na Temeke zilizoshiriki
mashindano hayo.

Kwa timu ya wanaume washindi ni Kinondoni pointi 10 wamepewe zawadi
ya Shilingi laki tatu na kombe kubwa.

Washindi wa pili ni Ilala baada ya kuibuka na pointi nane ambao
waliondoka na kikita cha shilingi laki mbili na Temeke walikuwa tatu
katika mashindano hayo, baada ya kupata pointi sita na walizawadiwa
shilingi laki moja.

Kwa upande wa timu ya wanawake washindi ni Ilala baada ya kupata
pointi tano, Temeke walishika nafasi ya pili walioshinda pointi tatu
na Kinondoni waliambulia patupu.

Washindi wawili wawili wanaume ni Alikhani Wallni, Bakeshi Salonk,
Uwari Habib na John Hezroni, kwa upande wa wanawake ni Iren Kihupi

Mashindano hayo yaliandaliwa na Chama cha Darts Mkoa wa Dar es Salaam
(Dada), yalishirikisha timu za zilizo katika wilaya ya Temeke, Ilala
na Kinondoni za wanaume na wanawake.

Katika mashindano hayo pia yalishirikisha wachezaji binafsi, mmoja
mmoja na wachezaji wawili wawili na washindi waliondoka na zawadi
iliyotolewa na wadhamini hao.

Mgeni rasmi alikuwa ni mwakilishi wa Mauzo wa TBL, Kanda ya Kinondoni
Endrew Misama.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...