Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, June 8, 2012

Mabondia wapima uzito kuzipiga FRIENDS CORNER HOTEL kesho





FADHILI MAJIA ambae ni bingwa UBO international na bingwa wa taifa wa
flyweight-PST 2012, TPBO 2010,TPBC 2009 na chalenger wa ubingwa wa
dunia wa WBO Afrika 2009 south Afrika amepima uzito na afya kiujumla

kwa ajili ya kumkabili mpinzani wake NASIBU RAMADHANI ambae ni bingwa
wa WBF(World Boxing Forum International Flyweight Title
) 2011.
Zoezi zima la upimaji lilisimamiwa na TPBO likiongozwa na IBRAHIM
KAMWE na kusema ya kuwa mabondia wote wapo katika afya njema na uzani
wao wote wamepata 50.8kgs kwa pamoja hivyo wapo sawa kupigana kwa
mujibu wa sheria za ngumi.
Tukumbuke majia alikwishawahi kuwa bingwa wa ubingwa huu mwaka 2008 na
kuucha na kwenda kugombania ubingwa wa dunia south Afrika na hivyo
kukaa bila kuutetea na kuchukuliwa na Haji juma wa Tanga,kwa sasa upo
wazi na unagombewa tena na majia mwenyewe na nasibu Ramadhani bondia
chipukizi na asiyepigika karahisi.
Katika mpambano huo pia kutakuwa na mapambano ya utangulizi kama
ifuatavyo na uzani wao waliopimaleo katika mabano -Abdala
mohamed"prince naseem"(63kgs) aataminyana na seba temba(64kgs) wa
morogoro raundi6,venas mponji(58.5kgs) na Amos mwamakula(60kgs),
Yohana Robert(62kgs) na Badi mombasa(61), Kasim mbundike(57kgs) na
Epson john wa morogoro(57.8kgs), iddi mnyeke 63 na Fadhili awadhi 63
mapambano yanategemewa kuanza saa kumi na moja jioni katika ukumbi wa
FRIENDS CORNER HOTEL 

 Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis na wengine kiba DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D
.

--
Super D Boxing Coach
Email.superdboxingcoach@gmail.com
www.burudan.blogspot.com
www.superdboxingcoach.blogspot.com
 Mob;+255787 406938
        +255774406938
        Po.Box. 15493
Dar es Salaam Tanzania

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...