Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 7, 2012

MASAWE MTATA AANZA KUREKODI VIDEO YA WIMBO WAKE WA UONGO KWELI


 MSANII maarufu wa vichekesho, anayeigiza na kundi la Ze Comedy kupitia Televisheni ya Chanel 5, Masawe Mtata 'Kicheko', ameanza kurekodi video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Uongo Kweli.

Masawe Mtata, ameanza video ya wimbo huo jana na anatarajia kumaliza kesho siku ya ijumaa chini ya Mwongozaji wake 'Pete'.

Aidha Masawe anayetarajia kukamilisha video ya wimbo huo mwezi ujao, amesema kuwa anatarajia kuanza kuachia Cd ya wimbo wake huo mara tu baada kukamilika kwa video hiyo ambapo atasambaza katika vituo mbalimbali vya redio na Televisheni kwa pamoja.

Wimbo huo ni mmoja kati ya nyimbo sita zitakazokuwemo katika albam yake mpya anayoendelea kuiandaa ambapo tayari amekwisharekodi nyimbo mbili.

Aliutaja wimbo alioanza kurekodi kuwa ni Nipe kidogo nichangamshe damu, ambao amemshirikisha Rapa mahiri Sauti ya Radi, huku wimbo huo wa Uongo Kweli ukiwa ni wapili.

Masawe amesema kuwa katika albam yake hiyo ambayo anaamini itamtambulisha vyema katika Jukwaa la Muziki, huku akitumia staili yake ya Bongo Tekno, anatarajia kuwashirikisha wakali kadhaa wa muziki wa dansi na wa muziki wa Bongo Flava wa nchini iwapo watakuwa tayari kukubali kumpa shavu katika kumtambulisha katika anga za muziki huo.

Kuhusu sanaa yake ya vichekesho anayoendele nayo katika kundi la Ze Commedy, Maswe alisema kuwa anaendelea kupiga mzigo na kundi lake hilo huku akiendelea kufanya kazi za nje ya kundi hilo ambayo ni kutambulisha kipaji alichonacho kwa mashabiki wake, ambapo ameahidi kufanya mambo makubwa ya  kuwashanga na kuwashitua wakali wa muziki nchini.

''Sanaa yangu ya kuigiza na kuchekesha siwezi kuancha ninaendelea kama kawaida na ndiyo maana natumia zaidi sauti yangu ya Masawe Mtata katika baadhi ya nyimbo zangu nitakazorekodi, ili niweaze kuwaonyesha mashabiki wangu kuwa kipaji nilichonacho katika vipande vyangu vya Mazuzu ni uwezo binafsi, kutokana na kipaji nilichonacho. alisema Masawe

Aidha Masawe alisema kuwa anatarajia kurekodi baadhi ya nyimbo zake zilizobaki katika Studio za Magic Star zilizopo Sinza na nyingine kurekodi katika studio tofauti ili kuleta radha tofauti ya muziki na nyimbo zote zitakazokuwamo katika albam yake hiyo.

 Wanenguaji wa kike wa kundi la Masawe Mtata, wakiwajibika jukwaani wakati wa zoezi la kurekodi video ya wimbo huo.
 Masawe Mtata, akiwapagawisha mashabiki wake waliofurika wakati akirekodi video ya wimbo wake wa Uongo Kweli.
Wanenguaji wa kiume na wa kike, wa Masawe Mtata, wakipozi kwa Picha wakati wakirekodi video hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...