Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 21, 2012

MASHABIKI WA CHEALSEA TANZANIA KUSHUSHA BONGE LA PATI MSASANI BEACH CLUB




 Christian Bella kulia na Rama wa kutoka Akudo Impact ambao ndio watakaotoa  burudani siku hiyo katikati anayezungumza ni Katibu Mkuu wa Chealsea Tanzania Cloford Ndimbo, mkutano huo umefanyika kwenye ukumbi wa Msasani Beach Club jijini Dar es salaam.
 Christian Bella kulia na Cliford Ndimbo wakionyesha bendera ya Klabu ya Chealsea ya Uingereza katika mkutano wa waandishi wa habari leo.
 
CHELSEA Tanzania leo imewatangaza wasanii watakaopamba sherehe za ubingwa zitakazofanyika kwenye ukumbi wa Msasani Beach Club Jumapili hii.
Mbali na michezo itakayozikutanisha Chelsea Tanzania ,Arsenal Tanzania na Manchester United Tazania pia kutakuwa na burudani mbalimbali wakiwemo Mr.Nice,Sweet Sunday,Muumin Mwinyjuma,Charlesa Baba,Shilole atakayesindikizwa na Irene Uwoya na Akudo Impact.
Kiingilio kitakuwa shilingi elfu 10 kwa wakubwa na watoto shilingi elfu 1.
Sherehe hizo zitaanza tokea saa 4 asubuhi kwa soka la ufukweni.
Sherehe hizo ni mwanzo tu wa mambo mengi makubwa yatakayofuata baada ya usajili wa Taasisi itakayotambulika pia makao makuu huko London.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...