Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, June 15, 2012

MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS BADO INAENDELEA


 Timu ya wasichana Arusha wakifurahia ushindi baada ya kuwafunga timu ya kinonodoni wasichana mabao 2 – 0  jana katika michuano ya Airtel Rising Stars inayofanyika katika viwanja vya Karume jijini Dar es Saalam

Mwenyekiti wa DRFA Amin Bhakresa akiongozana na Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde wakisalimia na timu za wasichana kabla ya kuanza mechi thidi ya timu ya wasichana wa Arusha na Mbeya katika michuano ya Airtel Rising Star inayofanyika katika viwanja vya Karume jijini Dar es Saalam. Katika mechi hiyo Mbeya iliifunga Arusha 3-2

Michuano ya Airtel Rising stars bado inaendelea ambapo jana timu za Temeke zilishindana na timu ya ilala na kisha kufatiwa na timu za Kinondoni kuchuana na timu za Arusha

Matokeo yaikuwa kama ifuatavyo Ilala wasichana walishinda 2 na temeke0 na kwa upande wa wavulana Temeke walishinda 3 na ilala 0, katika mechi zidi ya Kinondoni na Arusha ,

timu ya Arusha wasichana ilshinda bao 2  kwa 0 thidi ya Kinondoni na kwa upande wa wavulana Arusha ilishinda 3 na huku Kinondoni ikiondoka na mabao 2. Michuano bado inaendelea Leo  siku ya Alhamishi Asubuhi Ilala itachuana na LindiNa ijumaa itakuwa nusu fainali kati ya timu zitakazoshinda kwenye magroup yao

siku ya Jumapili ndiyo itakuwa finali ya mashindano hayo ambapo timu itakayoshinda itapata nafasi ya kushiriki mashindano ya Africa – intercontinental tournament ambayo yatakayofanyika mwenzi wa nane nchini Kenya, na pia katika fainali hiyo wachezaji sita nyota watachaguliwa kujiunga na clinic chini ya mafunzo makocha wa klabu ya Manchester united inategemea kufanyika pia mwenzi wa Agasti nchini Kenya

Wote mnakaribishwa kushuhudia michuano hii inayofanyika katika viwanja vya karume kila siku,  kiingilio ni bure,  njooo ushuhudie mashindano haya ya Airtel Rising stars yenye hamasa na muamko mkubwa

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...