Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Wednesday, June 6, 2012

MKURUGENZI ATCL AFUKUZWA KAZI



DAR ES SALAAM, Tanzania
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe ametengua nafasi ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Paul Chizi kutokana na uteuzi wake kuwa kinyume na sheria, Kanuni na Utaratibu wa Utumishi wa Umma .

 Aidha Waziri Mwakyembe pia amewasimamisha kazi maofisa wanne wa Kampuni hiyo akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Fedha wa ATCL.

 Kwa mujibu wa taarifa iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Omary Chambo, kutenguliwa kwa nafasi hiyo kuanzia  Juni tano.

“Chizi Paul aliteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege (ATCL) Agosti  6 mwaka 2011, hata hivyo utaratibu wa uteuzi wake haukufuata Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma”ilisema taarifa hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...