Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, June 1, 2012

MKUTANO WA SHIRIKISHO LA NGUMI LA DUNIA IBF WAENDELEA HUKO HONOLULU MAREKANI


 
Rais wa IBF/USBA duniani Daryl Peoples wa Marekani kushoto akiwa amesimama na Rais wa IBF bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi siku ya ufunguzi wa mkutano huo tarehe 31 May, 2012.
Rais Peoplers aliwakaribisha wajumbe na kuwasomea taarifa ya mwaka ya IBF/USBA ambapo zaidi ya mapambano ya ubingwa 349 yalifanyika chini ya IBF/USBA mwaka jana. 
 
Mkutano huo ulihutubiwa pia na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi. Aidha mwakilishi wa IBF katika bara la Ulaya Roberto Reya wa Italia naye alihutubia mkutano huo.
 
Katika mkutano huo taarifa ya kifo cha bondia wa Thailkand Thangthong Kiattaweesuk aliyekuwa na miaka 35 kilitolewa rasmi. Bondia Kiattaweesuk alikufa katika ajali ya gari akiwa na mkewe, mtoto mmoja na ndugu yake baada tu ya kushinda pambano lililompa nafasi ya kupigana na bingwa wa IBF wa dunia katika uzito wa Feather Geoffrey Mathebula wa Afrika ya Kusini.
 
Kiattaweesuk alimpiga bondia wa Kenya Geofrey Munica kwa KO raundi ya 10 katika pambano la kugommbea mkanda wa mabara wa IBF.
 
Pamoja na ufunguzi huo leo kutakuwa na semina ya utibabu pamoja na semina ya majaji. Mkutano huo utamalizika tarehe 2 Juni.
 
Mkutano huu unahudhuriwa na wajumbe 6000 toka nchi 204 duniani kote. Ujumbe wa Afrika ni moja ya ujumbe unaoshiriki katika mkutano huu maalum wa kuafiki programu ya Utalii wa Michezo itakatowakilishwa na Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...