Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, June 8, 2012

MWALIMU SHULE YA MSINGI KIHESA NUSURU AMTOE JICHO MWANAFUNZI KWA BAKORA


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dr.Shukuru Kawambwa
MWALIMU wa shule ya msingi Kihesa, Manispaa ya Iringa anatuhumiwa kumpiga mwanafunzi na kumsababishia maumivu makali sehemu yake ya jicho.
Mwandishi wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka mkoani Iringa ZAHRA SULEIMANI anaripoti kuwa tukio hilo limetokea leo .

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo shuleni hapo mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kihesa Manispaa ya Iringa Bw.ZABIHU HASSAN amesema tukio hilo limetokea baada ya mwalimu kutoa adhabu kali kwa mwanafunzi wake.
Mwalimu HASSAN amewakumbusha walimu wa shule za msingi kupunguza na kuacha tabia ya kutoa adhabu ukali wa wanafunzi na badala yake wametakiwa kutoa adhabu zitakazoweza kuwanufaisha wanafunzi katika taaluma.
Mzazi wa mwanafunzi huyo FATMA KIGUDA amesema lazima serikali kuangalia upya suala la adhabu ili sheria iweze kuchukua nafasi na iwe fundisho kwa walimu wengine ili waweze kujifunza.
Hata hivyo, mwalimu ambaye ametenda kosa hilo ambaye amefahamika kwa jina la Mwalimu KIFYOGA amekanusha madai hayo na kusema kuwa hakukusudia kufanya tukio hilo bali ni sehemu ya maonyo kama wanafunzi wengine.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...