Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, June 8, 2012

NABAKI AFRIKA YATOA MILIONI 15 KWA MSHINDI WA DROO YA SHINDA PAA KUTOKA NABAKI AFRIKA


Mkurugenzi mkuu wa Nabaki Afrika  Ltd Bw. Hamish Hamilton akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kukabidhi hundi ya kiasi cha shilingi 15.000.OOO, kwa mshindi wa droo iliyochzeshwa na kampuni hiyo mei 31 mwaka huu. Nabaki Afrika ilikabidhi hundi hiyo kwa Bw. Kalembo Bisaya ambaye ndiye mshindi wa Droo hiyo ambapo kila mmoja wa wateja hawa wamenunua  aidha vifaa vya mfumo wa kuvuna maji ya mvua  vijulikanavyo kama Marley Gutters au mfumo wa kuzuia joto katika paa pamoja na  vigae vya kuezekea aina ya DECRA. Washiriki katika shindano hilo walikuwa 101 ambapo amesema wateja wote ambao wamenunua vigae vya DECRA wataweza kuona tofauti nzuri ambayo ni DECRA halali tu ndiyo inatoa. Makabidhiano hayo ya hundi yalifanyika katika makao makuu ya Nabaki Afrika leo Jijini Dar es Salaam.
Mshindi wa Droo hiyo Bw. Kalembo Bisaya akizungumza na waandishi wa habari juu ya furaha yake baada ya kukabidhiwa hundi hiyo.
Mkurugenzi  mkuu msaidizi wa Nabaki Afrika  Ltd Bi. Tamia Hamilton akifafnua juu ya utoaji wa zawadi hizo kwa wale wateja waliofanikiwa kushinda katika Droo hiyo.
Bw. Alison Malopa ambaye ni meneja mauzo na maonyesho katika kampuni ya Nabaki Afrika akifafanua juu ya droo hiyo ambayo alisema ni ya mwisho katika shindano hilo linalokwenda kwa jina la Shinda paa.
Bw. Kalembo Bisaya akiwa kwenye picha ya pamoja na mkewe bada y kupokea hundi hiyo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...