Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, June 17, 2012

NBC YAITANDIKA BACLAYS GOLI 4-3 VIWANJA VYA TCC CHANG'OMBE


Mchezaji wa timu ya soka ya NBC,  Hussein Shabani (kulia)
akigombea mpira  na Henry Justin wa timu ya Barclays katika mechi ya
kirafiki  iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. NBC ilishinda kwa
penalti 4-3 baada ya kutoka sare ya mabao 2-2.
Wachezaji wa timu ya soka ya NBC wakishangilia baada ya kuibuka
kidedea kwa kuinyuka timu ya Barclays kwa mabao 4-3 katika mchezo wa
soka wa kirafiki jijini Dar es Salaam mwishoni leo.
Mchezaji wa timu ya soka ya NBC,  Ibrahim  Makoye (kulia)
akimiliki mpira mbele ya Khatibu Shilumba wa timu ya Barclays katika
mchezo wa kirafiki  uliofanyika katika Viwanja vya TCC Club,
Chang’ombe, Dar es Salaam leo. NBC ilishinda kwa penalti 4-3.
Mkurugenzi wa Technolojia Habari wa Barclays, Dakshit Pandya
(katikati) akikabidhi kikombe cha ushindi wa kwanza kwa nahodha wa
timu ya soka ya Benki ya NBC baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-3
katika mchezo wao wa kirafiki uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.
Kulia ni Mkuu wa Idara ya Technolojia Habari (IT) wa NBC, Pete Novat.

Mkuu wa Idara ya Teknolojia Habari (IT)  wa Benki ya NBC,  Pete
Novat(kulia) akikabidhi kikombe cha ushindi wa pili kwa nahodha wa
timu ya soka ya Barclays, Siaga Mgweno mara baada ya mechi ya kirafiki
baina ya timu za benki hizo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo. NBC
ilishinda kwa penalti 4-3. Katikati ni Mkurugenzi wa IT wa Barclays,
Dakshit Pandya.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...