Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, June 3, 2012

SHIRIKISHO LA NGUMI LA KIMATAIFA (IBF) LAMKUMBUKA NA KUMLILIA BONDIA MAGOMA SHABAN



SHIRIKISHO la Ngumi la Kimataifa (IBF) pamoja na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) vyatuma salamu za rambirambi na kumlilia bingwa wa IBF wa mabara na bingwa wa dunia wa WBU Magoma Shaban.

Magoma aliyefariki jana katika hospitali ya Bombo jijini Tanga atakumbukwa kwa umahiri wake katika mchezo huo wa ngumi za kulipwa.

Safari ya Magoma Shaban kwenye ngumi za kulipwa ilianzia katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga mwaka 1998 wakati Onesmo Ngowi akiwa ndio kwanza ameteuliwa na Rais wa zamani wa IBF Robert Lee Sr, kutoka nchini Marekani kuanzisha shirikisho hilo la IBF katika bara la Afrika.

Katika pambano hilo lililofanyika uwanja huo wa Mkwakwani, Magoma Shaban, alipigana na Joseph Waweru kutoka Kenya na kumshinda kwa KO na kutangazwa kuwa bingwa wa IBF katika bara la Afrika uzito wa Flyweight.

Mwaka 2000 Magoma chini ya kamouni ya Capital Promoters Limited chuini ya mwandishi wa bahari mahiri bwana Gabriel Nderumaki alipigana na bondia Totim Lukunim toka Thailand katika ukumbi wa PTA kugombea mkanda wa IBF wa mabara katika uzito wa Flyweight na kumshinda  kwa KO katika raundi ya 4. Huo ndio ukawa mwanzo wa magoma Shaban kwenye kwenye matawi ya juu katika ngumi.

Magoma Shaban alipigania ubingwa wa dunia wa WBU nchini Italy na kumshinda bondia Ferid Ben Jeddou kwa TKO katika raundi ya 6.

Magoma alikuwa ni bondia aliyeing'arisha Tanzania na bara zima la Afrika katika medani ya ngumi za kulipwa duniani.

Kwa mantiki hiyo leo IBF imetangaza rasmi kuuita mkanda wa uzito wa Fly aliokuwa anachezea Magoma kuwa "Mkanda wa Magoma Shaban" katika mapambano yote yatakayokuwa yanachezezwa katika uzito huu yatajulikana kama "Ubingwa wa IBF Africa wa Magoma Shaban".

Tunafanya hivi ili kuwaenzi mabondia wanaoleta mchango mkubwa katika medani ya ngumi na hivyo majina yao kubakia katika kumbukumbu zetu milele.

Mola alitoa na Mola ametwa, jina lake lihidimiwe milele. Amin!

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...