Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, June 3, 2012

Shoo ya Dogo Aslay live Dodoma .Ferooz kuwachezesha Kibodaboda


 Na Mwandishi Wetu

MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Ferouz Mrisho ‘Ferooz’ ameahidi kuwachezesha mtindo wake wa ‘Kibodaboda’ mashabiki watakaohudhuria onyesho la kumtambulisha Aslahi Isihaka ‘Dogo Aslay’ litakalofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Jumamosi ya Juni 9, mwaka huu.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana Ferooz ambaye hivi sasa anatikisa kwa sana na nyimbo zilizo kwenye albamu yake mpya ‘Rizevu’ zilizo kwenye mahadhi ya mchiriku alisema kuwa mashabiki wa mjino Dodoma watapata bahati ya kuwa wa kwanza kuzisikia nyimbo zote mpya ambazo baadhi bado hazijasikika hata kwenye redio.
Alisema kwamba amepania vilivyo kuwaonyesha wakazi wapenzi na mashabiki wake namna ya kucheza ‘Kibodaboda’ mtindo uliotokea kukubalika na kuifanya albamu yake mpya aliyoitoa hivi karibuni kuwa gumzo.
“Ninawaambia wapenzi wa wangu na wapenzi wa bongo fleva kwa ujumla wa Mkoani Dodoma wasilikose onyesho la Dogo Aslay Live kwani nimewaandalia vitu ambavyo hawatavisahau, nitaimba nyimbo zangu zote mpya na nitawaonyesha jinsi ya kucheza ‘Kibodaboda’,” alisema Ferooz.
Msanii huyo aliyepata kutamba na wimbo wa ‘Starehe’ kwa sasa anatamba na wimbo wa ’Ndege Mtini’, ulio kwenye albamu ya ‘Rizevu’ aliomnshiriki Shoz Dia wa Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT), pia nyimbo nyingine ni kama:  ‘Tusitafutane’ aliomshirikisha Abbas Hamisi ‘20 Pacent’, ‘Sio Ize’ na ‘Rizevu’ uliobeba jina la albamu.
Naye Mratibu wa onyesho hilo Jackline Masano, alisema mbali ya Ferooz, wasanii wengine watakaotumbuiza ni pamoja na wasanii kutoka kituo cha kuibua vipaji cha Mkubwa na Wanawe cha Temeke Sandali, jijini Dar es Salaam kilichomuibua Dogo Aslay.
“Pia kutakuwa kundi zima la TMK Wanaume Family la Temeke jijini Dar es Salaam, Mfalme wa Rhymes nchini Selemani Msindi ‘Afande Sele’ na 20 Pacent kutoka Morogoro, kiingilio kitakuwa sh 3,000 kwa kila mmoja atakayeingia kwenye uwanja wa Jamhuri na onyesho hilo litaanza saa 6:00 mchana hadi saa 12:00 jioni, lakini saa 2:00 usiku hadi 6:00 usiku, wasanii hao wote watahamishia burudani kwenye ukumbi wa Royal Village mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...