Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, June 14, 2012

SIJAIKACHA BENDI YA MAPACHA WA3 NIMEAMUA KUPUMZIKA NACHEZA BASKET BALL- KALALA JUNIOR


 Kalala Junior, akiwa katika mazoezi ya mpira wa Kikapu na timu yake ya Oilers, yanayofanyika kwenye Viwanja vya Leaders Club.

Kalala Junior
 MWIMBAJI mahiri na mmoja wa Wakurugenzi wa bendi ya Mapacha wa3, Kalala Junior, amesema kuwa yote yanayosemwa na baadhi ya watu na yanayoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari yamekuzwa tofauti na ukweli kuhusu kupumzika kwake katika bendi hiyo.

Kocha wa Kalala, Mziray Kinje
Siku chache zilizopta Kalala, aliripotiwa kuipa kisogo bendi yake hiyo, kwa kile kilichoelezwa kutokea mtafaruku wakutoelewana na mwenzake Jose Mara na Mpiga Solo wao, Allan Kiso Mundele, huku ikielezwa kuwa mapacha hao waili Jose na Kalala walifikia hatua ya kushikana mashati wakitaka kuzichapa kavukavu.

Mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, umezungumza na mkali huyo Kalala Junior, ambaye ameamua kufunguka na kuweka 
wazi ukweli kuhusu jambo hilo na tukio lenyewe linaloelezewa tofauti.

Sufianimafoto, alikukutana na Kalala, katika foleni ya magari eneo la Kituo cha Studio, na mafoto ilipojaribu kumdadisi Kalala, alisema kuwa asingeweza kuzungumza kwani alikuwa akiwahi kwenye mazoezi ya Mpira wa Kikapu na timu yake ya Oilers, inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza ngazi ya Mkoa wa Dar es Salaam, inayojifua katika Viwanja vya Leaders Club.

Mafoto, iliamua kugeuza gari na kuongozana na Kalala, hadi Leaders ili kujua kulikoni, mkali huyu kuamua kuacha muziki na kujikita katika mchezo wa mpira wa Kikapu.

Baada ya kufika katika viwanja vya Leaders, Mafoto ilimshuhudia Kalala, akijumuika na wachezaji wenzake wa timu hiyo ya Oilers, huku wakiongozwa na Nahodha wa timu hiyo, ambaye pia ni Nahodha wa timu ya Taifa ya Mpira wa Kikapu, Lusajo Samwel, huku timu hiyo ikiwa ni chini ya Kocha wake, William Mziray 'Kinje'.

Kalala, alisema kuwa timu yake hiyo iko katika mazoezi makali ya kujiandaa na mchezo wake dhidi ya timu ya Magone, mchezo utakaochezwa siku ya jumapili saa sita mchana Uwanja wa ndani wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mtandao huu, Kalala, alisema kuwa amekuwa akisikia mengi kuhusu kupumzika kwake jambo ambalo amesema si kweli. 

Akifungika zaidi Kalala, amesema kuwa yeye ameamua kupumzika kwa kipindi cha mwezi mmoja na nusu baada ya kujihisi kuchoka kwa kufanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika, kama ambavyo alifanya Jose Mara siku za hivi karibuni.

''Mimi nimeamua tu kupumzika kwani nimechoka na nimefanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika, hayo yanayosemwa na watu wala si ya kweli, mimi na Jose tulitofautiana tu katika mazingira ya kazi wala hatukupigana kama inavyoelezwa, kama unavyojua mimi ni kiongozi katika bendi sasa inapotokea mwenzio amekosea ni lazima kumweleza ukweli na ndiyo iliyotokea, kwani kama unavyofahamu mtu unapokuwa tayari damu imechemka huwezi zungumza taratibu, basi watu wakahisi tunagombana jambo ambalo si la kweli,

Na pia sijagombana na wenzangu, nasisitiza kuwa nimeamua kupumzika na nitakapokamilisha siku zangu za mapumziko nitarejea kazini kama kawaida, na juzi tu nimezungumza na wenzangu na wanatambua mapumziko yangu, hao wanaosema nataka kwenda Twanga, sijui Mashujaa, mara Extra Bongo, ni wazushi tu, sina mpango wa kufanya hivyo na iwapo itatokea kufanya hivyo basi ni mimi ndiye wa kutoa taarifa hizo,

Katima muda wangu wa mapumziko nimeamua kujishughulisha na kujiweka bize na mazoezi ya Mpira wa Kikapu, wala si kweli kuwa nimeamua kuacha muziki na kuamua kucheza kikapu, haya ni mazoezi tu ikiwa ni pamoja na kutafuta pumzi zaidi''. alisema Kalala
Kalala (katikati) akiwa katika mazoezi na wachezaji wenzake wa timu ya Oilers.

Kalala (katikati) akiwa katika mazoezi na wachezaji wenzake wa timu ya Oilers. zaid tembelea http://sufianimafoto.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...