Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 5, 2012

TBL YAMZAWADIA BAJAJ MSAMBAZAJI BORA KANDA YA KUSINI


Meneja Mauzo na Usambazaji wa Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL), Kanda ya Kusini, James Bokela (wa
pili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa
Kampuni ya Massawe Glosery, Jacob Massawe (wa pili
kulia) ufunguo wa Bajaj yenye thamani ya sh. mil.
4.7, baada ya kuwa mshindi wa kwanza wa kanda
hiyo kwa usambazaji na uuzaji wa bidhaa za TBL.
Wanaoshuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika
Kibaha, Pwani juzi, ni mke wa Massawe, Anna
Massawe na Meneja wa Huduma za Biashara wa TBL,
Reginald Mosha
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Massawe
Glosery, Jacob Massawe (wa pili kulia) na mkewe
Anna Massawe wakifurahia zawadi ya Bajaj
yenye thamani ya sh. mil. 4.7.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Massawe
Glosery, Jacob Massawe (wa pili kulia) na mkewe
Anna Massawe (kulia), wakifurahia zawadi ya Bajaj
yenye thamani ya sh. mil. 4.7, kwa kugongeana
chupa na baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL) na wamiliki wa baa wilayani  Kibaha,
waliyokabidhiwa na TBL, baada ya kampuni yao kuwa
washindi wa kwanza Kanda ya Kusini kwa usambazaji
na uuzaji bora wa bidhaa za TBL. Hafla hiyo ilifanyika
Kibaha, mkoani Pwani juzi.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...