Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 5, 2012

TWANGA WAJIGAMBA WAO NI ALFA NA OMEGA,KUZINDUA KAMPENI YA TWANGA AMSHAAMSHA CLUB BILICANAS J5





  KUTOKA Kulia ni mwimbaji wa bendi ya Twanga pia Kiongozi Luizer Mbutu, Mkurugenzi Asha Baraka na mwimbaji Sleh Kupaza wakiwa katika mkutano na Waandishi wa Habari hawapo pichani leo mchana katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mango Garden Kinondoni, Jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Dande Junior)
UONGOZI  wa bendi ya Twanga International  ‘Kisima Cha Burudani’ jana wametangaza mpango wao wa kuanzisha kampeni ya kujitangaza ya amshaamsha ya Twanga katika ukumbi wa Club  Bilicanas itakayozinduliwa rasmi kesho.
Alisema katika onesho hilo litakaloanza milango ya saa tatu usiku kiingilio kitakuwa ni sh. 8,000 kwa kila mtu. 
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Twanga International Asha Baraka ambapo pia alisema bendi yao wameamua kuanzisha kampeni hiyo  kwa kupiga muziki katika mtindo wa ‘Non Stop’ yaani watakuwa wakipiga muziki kuanzia saa tatu wakati onesho linapoanza hadi kunapokucha.
“Aidha napenda kuchukua fursa hii kuwatangaza msemaji mpya wa bendi hii ambaye ni mkongwe katika fani na medani ya muziki kwa ujumla Muddy Pizaro atakayekuwa akijibu kila kitu kinachoihusu bendi ya Twanga” alisema Asha.

Aidha aliwataja wengine waliopewa nyadhifa katika bendi hiyo ni pamoja na mwanamuziki ambaye ni kati ya waasisi wa bendi hiyo Hamisi Kayumbu ‘Amigolas’ aliyekabidhiwa mikoba ya kuwa Meneja wa wanamuziki wote katika bendi hiyo.
Asha aliongeza kwa kusema kuwa bendi yao bado iko imara kama chuma na wanajivunia kuwa wao ni sawa na shamba au mti wenye matunda kwani kwa sababu hizo imekuwa kwao ni kjambo kawaida kupopolewa.
“Sisi tulianzisha Twanga Academia leo matunda yake yanaonekana tunawanamuziki wengi hivyo hatuwezo kutetereka katika muziki kwa sababu ni jadi yetu hapa ni bandika bandua labda waninunue na mimi mwenyewe” alisema.
Baadhi ya wanamuziki waimbaji wanaokimbiza Twanga hivi sasa ni pamoja na Dogo Rama, Venace, Badi Bakule, Luiza Mbutu, Saleh Kupaza na Rapa machachari Greyson Semsekwa, na Msafiri Diouf.
Kama hiyo haitoshi pia alitambulishwa Muddy K ambaye atakuwa Meneja Matukio wa Twanga ambaye aliyekuwa katika  kempu ya Usher Family yenye maskani  yake  Temeke jijini Dar es Salaam.
Hivi sasa bendi hiyo inatamba na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Shamba la Twanga uliotungwa na Rapa Greyson Semsekwa na kutiwa nakshi na waimbaji wa bendi hiyo kwa ujumla.


 Wanenguaji wa bendi ya Twanga wakionesha umahiri wao katika  kuzungusha nyonga.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...