KAMPUNI ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania imewatahadharisha  wateja wao wa huduma ya M-pesa kuwa  makini kulinda namba zao za siri zisifahamike  na watu wengine, kuepuka kuibiwa fedha zao.

Akizungunza na waandishi wa habari juzi ofisini kwake Mlimani city Jijini Dar es salaam, afisa mawasiliano na mahusiano Joseline Kamuhanda ameelezea madhara yatokanayo na kuvuja kwa namba za siri za mteja, hali inayosababisha wizi.

“Ukweli mteja akitoa namba  ya siri kwa wakala ili amsaidie kumtolea pesa katika akaunti yake ni hatari, kwa vile itategemea wakala huyo atakuwa na uadilifu wa kiasi gani, lakini pia hata kwa mtu wa karibu kumpa  kufahamu namba ya siri si jambo jema “ alisema Kamuhanda.

Akizungunzia kuboreshwa kwa mtandao huo  alisema M-pesa imezidi kuimarika baada ya kuondoa tatizo la ‘network’ kusumbua wakati Fulani, hali ambayo ilileta malalamiko kwa wateja.

“Tatizo la mtandao kusumbua katika zoezi utumaji pesa na upokeaji halipo baada ya wataalam kulifanyia kazi kikamilifu na kuliondoa” alisema Kamuhanda.

Akisisitiza kuhusiana na huduma za M-pesa afisa mkuu wa biashara Dylan Lennox amewaomba wateja kuwa na utamaduni wa kutuza namba za siri ikibidi kuzibadilisha kila baada ya muda, kuzuia hata ndugu wa karibu au rafiki kuikariri namba hiyo.

“Kuna watu wapelelezi wa mambo anakuzoea inafikia kujua namba ya siri ya akaunti yako, siku  unataka kutioa  fedha katika akaunti yako unaambiwa huna fedha za kutosha, badala yake unalaumu Vodacom wamekuibia kitu ambacho si kweli” alisema Lennox.

Alisema tatizo la mteja kuibiwa linahusiana na yeye mwenyewe kutoficha namba ya siri pengine kwa kutofahamu vyema namna ya njia za utoaji fedha kwa njia ya M-pesa, bila kujua  huyo aliyempa  namba ya siri  ameikalili na kutumia kumuibia.

Lennox anamalizia kwa kusema  kuwa Voda com imejipanga vizuri zaidi kwa ajili ya kuwapa watanzania na wateja wote kwa ujumla kuwapa huduma bora za kisasa ili kujiendeleza katika masuala ya kiuchumi na kijamii na kuwaomba watanzania waitumie vizuri huduma mpya ya wajanja.