Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, June 15, 2012

WABONGO WAWILI WASAFIRISHWA KWENDA IRAN KWA MASHINDANO YA KUSOMA KURUAN



KITUO cha Utamaduni cha Jamhuri ya Irani jana kimewasarifisha vijana wawili wa Kitanzania kwenda Iran kwa ajili ya Mashindano ya Kimataifa ya Kusoma Kuruan yatakayoshirikisha nchi 40.
 
Akizungumza wakati wa kuaga vijana hao, Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alisema vijana hao wanapaswa kuwa makini katika mashindano hayo kwani wamebeba bebndera ya nchi.
 
Alisema safari hiyo imegharimiwa na nchi ya Iran ambapo vijana hao wakati wakiwa nchini humo kwa muda wa juma zima huduma zote za kijamii zitakuwa juu yao.
 
Alhad Salum aliwataja vijana hao kuwa ni Saidi Idd Saidi na Omar Salumu ambapo Saidi anatarajiwa kushiriki katika shindano la kusoma ,Tajuwid’ huku Salumu akishiriki katika kosoma Kuruan ambapo shindano hilo litafanyika juma lijalo.
 
Alisema vijana hao walipata fursa hiyo baada ya kushinda katika shindano lililoandaliwa kwa kuwakutanisha na wenzao kutoka vyuo na taasisi mbalimbali hapa nchini.
 
“Leo tunawaaga vijana hawa na tunaamini kuwa wataenda kufanya vizuri na watarudi wanang’ara kwa kupata ushindi”alisema Salum.
 
Alhad Salum anatarajia kuwa safari hii vijana hao watarudi na ushindi wakwanza ukilinganisha na ule wa mwaka jana, Tanzania ilishika nafasi ya pili.
 
Aidha, alisema anakishukuru kituo hicho cha Utamaduni kwa kuandaa mashindano hayo kila mwaka ambapo ni jambo zuri katika kuwajenga vijana katika maadili mema yatakayowakinga na vitendo viovu duniani.
 
Alisema kwa kila mwenye kuifahamu kuruan anapaswa kumfundisha mwingine kitendo ambacho ndicho kinachofanywa na nchi hiyo ya Irani.
 
Naye Mkurugenzi wa Kituo hicho Morteza Sabouri aliwaasa vijana hao kwenda kufanya kile kinachowapeleka huko kwani watambuwe nafasi hizo ni adimu ukichukulia wapo vijana wengi wenye uwezo kama wao hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...