Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, June 12, 2012

WAKAZI WA IRINGA WAJITOKEZA KWA WINGI KUSHUHUDIA UZINDUZI WA HUDUMA MPYA YA AIRTEL JIUNGE NA SUPA5



Mmoja wa wakazi wa Iringa aitwaye Theresia Mifwa akikabidhiwa simu ya mkononi aina ya sumsung na Meneja Mahusiano wa  Airtel-Tanzania,Jackson Mmbando, mara baada ya kuichambua vyema huduma ya Jiunge na Supa5 kwa ufasaha ,wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Jiunge na Supa5 uliyofanyika jana kwenye uwanja wa Mwembe Togwa mkoani Iringa. Airtel Jiunge na Supa5 Ilizinduliwa kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam hivi karibuni.Ukitaka kujiunga na huduma hiyo ANDIKA SMS YENYE NENO ‘WIKI’  AU WIKI UTUME KWENDA 15548.
Kundi la wasani mahiri wa muziki wa kizazi kipya,lenye maskani yake Temeke,jijini Dar liitwalo Wanaume Halisi,likiongozwa na Sir Juma Nature,wakilishambulia jukwaa vilivyo jana jioni mbele ya umati wa wakazi wa Iringa waliojitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Mwembe Togwa,mjini humo na kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya airtel Supa5 yenye lengo la kutoa huduma tano nafuu za huduma za mawasiliano kupitia Airtel.huduma hiyo itaendelea kutambulishwa tena katika mkoa wa Arusha na baadaye jijini Mwanza.

Wakazi mbalimbali wa mjini Iringa wakiendelea kuhamia Airtel na kujipatia huduma mbalimbali zilizokuwa zikipatikana wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya airtel Supa5 yenye lengo la kutoa huduma tano nafuu za huduma za mawasiliano kupitia Airtel kwa wateja wake.

Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya (hip hop), aitwaye Roma akiwarusha baadhi ya Wakazi wa mji wa Iringa walijitokeza kwa wingi kwenye uwanja wa Mwembe Togwa,mjini humo na kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya airtel Supa5 yenye lengo la kutoa huduma tano nafuu za huduma za mawasiliano kupitia Airtel.huduma hiyo itaendelea kutambulishwa tena katika mkoa wa Arusha na baadaye jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...