Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, June 8, 2012

ZAWADI SBL ZARINDIMA MKOANI KILIMANJARO, WENGI WAKUSANYIKA KUSHUHUDIA WASHINDI WAKIKABIDHIWA ZAWADI ZAO.


Mkurugenzi wa masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Bw.Ephraim Mafuru wa pili kutoka kulia akikabidhi zawadi ya jenereta kwa mshindi wa promosheni ya vumbua hazina chini ya kizibo inayoendeshwa na kampuni hiyo hapa nchini, pamoja naye ni wafanyakazi wa kampuni hiyo tawi la Moshi mkoani Kilimanjaro.
Zawadi hizi zilikabidhiwa jana kwa washindi waliopatikana katika kitongoji cha kiboroloni na majengo mkoani Kilimanjaro. Picha ya pili ni Waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda mkoani humo wakimpongeza bodaboda mwenzao Bw.  Rogers kavishe abaye amejishindia jenereta  sambamba na Bw. Vicent  Lymo ambaye naye amejishindia jenereta.
 Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti Ephraim Mafuzu akihojiwa na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi zawadi ya jenereta kwa mshindi.
Bw. Deusdedit Tobias Njau 22akifurahia na wenzake mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake ya Jenereta.

Kampuni ya bia ya Serengeti jana imekabidhi zawadi ya jenereta mbili kwa washindi wa zawadi hizo katika kitongoji cha kiboroloni moshi mkoani Kilimanjaro ni katika promosheni ya VUMBUA HAZINA CHINI YA KIZIBO na SBL inayoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti.
Ni wiki ya 6 sasa kati ya wiki 16za promosheni hiyo ambapo katika droo ya sita iliyochezeshwa hivi karibuni washindi wawili walipatikana ambao ni Bw. Deusdedit Tobias Njau 22 kutoka kiboroloni mkoani Kilimanjaro ambaye alijishindia jenereta mpya na Bw. Vicent Lymo 36 kutoka kibosho mkoani Kilimanjaro ambaye amejinyakulia pikipiki mpya kabisa ambayo naye atakabidhiwa zawadi yake siku chache zijazo pindi taratibu za usajili zitakapokamilika.
Makabidhiano hayo yalifanyika jana na kupata kuhudhuriwa na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini huku tukio zima likishuhudiwa na umati mkubwa wa watu ambao walitoa maoni mabalimbali juu ya zoezi zima la promosheni hiyo na kusema SBL inabadilisha maisha ya watanzania wengi hasa vijana jambo ambalo linapaswa kuigwa na makampuni na mashirika mengine hapa nchini.Washindi hao wameishukuru SBL nakuitaka iendelee na moto huohuo.
Akiongea na waandishin wa habari wakati wa kukabidhi zawadi hizo Mkurugenzi wa masoko SBL Bw. Ephraim Mafuru amesema washindi hao walipatikana kihalali na kwamba kila mtanzania mweneye sifa zilizoainishwa katika vigezo na masharti ya promosheni hiyo ana haki na uwezo wa kushiriki na kushinda zawadi mojawapo au zaidi kati ya zawadi zilitajwa katika promosheni hiyo “leo tunawakabidhi hawa zawadi zao lakini siku chache zijazo tutakuwa hapa tena kwaajili ya kumkabidhi mshindi mwingine pikipiki mpya” alisema Mafuru na kuwataka watanzania wote wenye mapenzi mema na kampuni ya bia ya Serengeti waendelee kushiriki kwani batahi ya mtu haiwezi kwenda kwa mwingine.
Hii ni droo ya sita wiki ya sita mfululizo ambapo bado takriban wiki 16 sasa ili kuisha kwa promosheni hiyo ya pekee na aya kwanza kutokea hapa nchini ambapo zaidi ya milioni 780 za kitanzania zinashindaniwa kote nchini

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...