Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, June 4, 2012

Ziara ya kusaka washiriki wa Epiq Bongo Star Search mwaka huu kuanzia mkoani Dodoma



Na Mwandishi Wetu
ZIARA ya kusaka vijana watakaoshiriki katika shindano la Epiq Bongo Star Search mwaka huu inaanzia mkoani Dodoma Juni 15 katika Ukumbi wa Royal Village.
 Akizungumzia ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Benchmark  Production Ritha Paulsen alisema kuwa washiriki wanatakiwa kufika katika ukumbi huo kuanzia saa 12 asubuhi.
 Alisema kuwa kampuni yake inatarajia kuchukua vijana watatu hadi watano kutoka mkoa huo watakaouwakilisha mkoa huo katika fainali zitakazofanyikia Dar es salaam.
 Alisema  kuwa wakiwa mkoani humo wanatarajia kuona vipaji vya wasanii wa kila aina kwa kuwa EBSS inalenga kukuza vipaji vya vijana wenye uwezo wa kuimba aina zote za nyimbo.
 “ Kama ambavyo imeshafahamika kuwa mwaka huu mshindi wa EBSS atapata kitita cha shilingi milioni 50 taslim hivyo ni kwamba tunawaomba wakazi wa mkoa wa Dodoma wenye vipaji kuja kwa wingi siku hiyo” alisema Ritha
 Ritha ataongozana na majaji wengine ambao ni Salama na Master Jay. EBSS mwaka huu imedhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...