Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, November 23, 2012

MBEKI MGENI RASMI MAJADILIANO YA UONGOZI AFRIKA DAR ES SALAAM LEO


 Rais Mstaafu wa awamu ya pili ya utawala huru wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki (kulia) akifafania jambo wakati wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu,
Cleopa David Msuya. Mbeki alikuwa Mgeni Rasmi katika mdahalo huo.
 Mwenyekiti wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo, ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mdahalo huo jijini Dar es Salaam leo.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Prof. Joseph Semboja, akizungumza katika mdahalo huo.
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili ya utawala huru wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki (kulia) akikiwa mwenye tabasamu wakati Mwenyekiti wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo ulioandaliwa na Taasisi ya UONGOZI Tanzania, Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya akitoa ufafanuzi wa majadiliano.
 Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya na Mwenyekiti wa Mdahalo wa Uongozi Afrika, pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya UONGOZI, Prof. Joseph Semboja (katikati) wakimsikiliza Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Afrika Kusini Ami Mpungwe ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara na Mwenyekiti wa Tanzanite One muda mfupi kabla ya kuwasili kwa Mgemi rasmi wa Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo. 
Mawaziri Wakuu Wastaafu wa Tanzania, Cleo David Msuya (kulia)  na Salim Ahmed Salim wakijadiliana jambo muda mfupi kabla ya kuanza Majadiliano ya duara kuzungumzia uongozi barani Afrika na changamoto za maendeleo.PICHA ZAIDI BOFYA FATHER KIDEVU BLOG.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...