Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Saturday, December 29, 2012

MATAYARISHO YA ZANZIBAR KUHAMA ANALOGIA KWENDA DIJITALI YAENDELEA


Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema matangazo ya mfumo wa Analogia yatazimwa rasmi katika Mikoa yote ya Zanzibar ifikapo Februari 28 mwakani ili kupisha mfumo mpya wa matangazo kwa njia ya Dijitali.
 Waziri wa habari, utamaduni, utalii, na Michezo Said Ali Mbarouk ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari maelezo kikwajuni mjini Zanzibar kuhusiana na matayarisho ya kuhamia katika mfumo mpya wa matangazo ya Dijitali.
  Amesema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Kamisheni ya Utangazaji Zanzibar (ZBC) zimeshauriana na kukubaliana kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iingie katika mfumo mpya wa Dijitali kwa awamu ambapo kwa zoni ya Zanzíbar imekubaliwa kuwa February 28 2013 ndio iwe mwisho rasmi wa matangazo ya Analogi.
 Waziri Mbarouk amesema Wizara yake haitozima mitambo ya matangazo ya Analogi ifikapo Disemba 31 bali itakachofanya ni kutangaza kwa pamoja matangazo ya Analogi na Digitali kwa mfumo unaojulikana kitaalamu kama SIMU L CAST hadi itakapofika muda rasmi wa kuhama mfumo wa Analogy.
 Akizungumzia matayarisho ambayo yamefanywa na Wizara yake katika kuukabili mfumo mpya wa Matangazo ya Dijitali Waziri Mbarouk amesema tayari wamejenga kituo cha usambazaji ishara(signals) katika eneo la Rahaleo kitakachokuwa na kazi ya kupokea na kusambaza ishara na mitambo ya uendeshaji.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...