Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, December 24, 2012

TPBC KUMALIZA MWAKA 2012 NA MAFANIKIO LUKUKI


 
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Nchini (TPBC) inamaliza mwaka 2012 na mafanikio lukuki ikiwa imeweza kuiletea nchi ya Tanzania mapambano makubwa ya kimataifa zaidi ya matano.
Haya ni mafanikio ambayo yanapaswa kusifiwa na watanzania wote wapenda maendeleo kwani kutokana na mapambano hayo nchi imeweza kujulikana kimataifa, vivutio vyake vya utalii vimeweza kujulikana, nchi imeweza kuwatengenezea vijana ajira, na kuweza kupunguza uhalifu kwa kuweza kuwapa vijana kazi kwani kukaa kwao bure ni kishawishi tosha cha kutumia nguvu zao kwa shughuli ambazo sio za maendeleo.
 Katika mwaka unaoishia Desemba 31, 2012, TPBC imeweza pia kuwapeleka nje mabondia zaidi ya 15 wakiiwakilisha nchi ya Tanzania ambako waliweza kuitangaza nchi ya Tanzania vizuri na kuwavutia wageni wakitalii na kuwekeza katika nchi hii inayojulikana kama kisiwa cha amani katika bara la Afrika.
 Aidha, TPBC imeweza kuhudhuria mikutano mitatu mikubwa ikiwa ni pamoja na mkutano wa Bodi ya Wakurugenzi wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC) katika jiji la London, Uingereza na ule wa mwaka wa  Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola uliofanyika nchini Bahamas.
 Kadhalika TPBC iliwakilishwa kwenye mkutano wa 30 wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chana cha Ngumi  Cha Marekani (IBF/USBA) uliofanyika katika jiji la Honolulu, jimbo la Hawaii nchini Marekani pamoja na ule wa Baraza la Ngumi la Dunia (WBC) uliofanyika pia katika mjiji la Las Vegas, nchini Marekani.
 Hapa nyumbani , TPBC iliweza kutoa vibali na kusimamia mapambano mengi yaliyofanyika katika miji ya Tanga, Dar-Es-Salaam, Morogoro, Songea, Mbeya, Morogoro na Arusha na kuweza kuwapatia mabondia wengi  wa kitanzania mikanda ya Kanda, Taifa na Afrika ya Mashariki, Kati na bara la Afrika.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...