Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Monday, March 18, 2013

DK.SHEIN ZIARANI KASKAZINI PEMBA.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk .Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi mbali mbali na wana CCM, alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Karume Pemba, akiwa katika ziara ya kikazi katika Mikoa ya Pemba, akianzia Mkoa wa Kaskazni .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk .Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Viongozi  wa  Ofisi ya Mkoa wa Kaskazini Pemba, alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Jamhuri Hall, alipofika kupata ripoti ya Mkoa , akiwa katika  ziara ya kikazi katika Mkoa huo iliyoanza jana kwa kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiangalia utengenezaji wa barabara inayojengwa kwa Kutumia Saruji, Mchanga na Kifusi,ili kuzuiya uhifadhi wa mazingira ya misitu, katika msitu wa Ngezi Mkoa wa Kaskazini Pemba,alipofanya ziara jana kuangalia maendeleo ya jamii.
Baadhi ya Viongozi  na Watendaji wa Ofisi za Mkoa wa kaskazini Pemba wakisikiliza Ripoti ya Utendaji kazi za Mkoa huo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk .Ali Mohamed Shein, katika ukumbi wa wa mikutano wa Jamhuri Hall, akiwa katika  ziara ya kikazi katika Mkoa huo. Picha na Ramadhan Othman Ikulu

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...