Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Friday, March 29, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ATEMBELEA TUME YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA (COSTECH) KIJITONYAMA


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Mkurugenzi wa Sayansi ya Uhai, Dkt. Flora Tibazarwa, wakati Makamu alipofanya ziara ya kutembelea katika maonyesho ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Kijitonyama leo kujionea maendeleo ya tume hiyo inayozalisha vijana wabunifu wa masuala ya kisayansi. Kushoto kwa Makamu wa Rais ni, Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya chupa ya dawa ya kuongeza virutubisho mwilini, Juice Lishe,(Morizella Juice) huku akimsikiliza Dkt. Modest Kapingu, kuhusu matumizi ya dawa hiyo, wakati Makamu alipofanya ziara ya kutembelea katika maonyesho ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Kijitonyama leo kujionea maendeleo ya tume hiyo inayozalisha vijana wabunifu wa masuala ya kisayansi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Rachel Mbuliza wa Kampuni ya Intern, wakati Makamu alipofanya ziara ya kutembelea katika maonyesho 
ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Kijitonyama leo kujionea maendeleo ya tume hiyo inayozalisha vijana wabunifu wa masuala ya kisayansi. Katikati mzungu ni Nicole Stabbs.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Mtafiti wa TEHAMA kutoka COSTECH, Rahma Bashary, wakati Makamu alipofanya ziara ya kutembelea katika maonyesho ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Kijitonyama leo kujionea maendeleo ya tume hiyo inayozalisha vijana wabunifu wa masuala ya kisayansi. Kulia ni, Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa namna ya kutumia simu ya mkononi kuunganisha huduma ya mtumiaji simu ili kupata taarifa ya mkulima kutoka kwa Gwaliwa Mashaka wa Kampuni ya Spendid Amos, wakati Makamu alipofanya ziara ya kutembelea katika maonyesho ya Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) Kijitonyama leo kujionea maendeleo ya tume hiyo inayozalisha vijana wabunifu wa masuala ya kisayansi. Kushoto kwa Makamu wa Rais ni, Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Makame Mbarawa. Katikati (kushoto) ni Viana Mulokozi na Gillsant Mlaseko.
 Viajana, Nassor Nyihirani (kushoto) na Raphael Martin wa kampuni ya Comasi, wakimuonyesha Makamu wa Rais jinsi ya kutunza kumbukumbu za mauzo kupitia njia ya mtandao walioyoibuni hivi karibuni, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika maonyesho ya Tume ya Sayansi na Teknolojia leo.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa maonyesho ya Kisayansi yaliyoandaliwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia, leo.
Makamu wa Rais, akionyeshwa Gari la Maabara inayotembea, wakati alipokuwa akitembelea katika maonyesho hayo leo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...