Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, March 21, 2013

MISS UTALII TANZANIA 2012/13 WATEMBELEA UKUMBI WA KIMATAIFA NA KISASA WA MAKUMBUSHO YA TAIFA (NATIONAL MUSIUM THEATRE).


 Washiriki wa Fainali za Taifa za mashindano ya Miss Utalii Tanzania 2012/13, jana  wametembelea Ukumbi wa kwanza na wa Kisasa na wa aina yake Tanzania ambao unamilikiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia kurugenzi ya mambo ya kale na makumbusho ya Taifa uliopo ndani ya Makumbusho ya Taifa jirani na Chuo cha Usimamizi wa Fedha(IFM) karibu na maeneo ya Ikulu jijini Dar es Salaam.

Wakiwa katika Ukumbi huo wenye uwezo wa kuchukua watu 470 kwa wakati mmoja, walishuhudia Viti, Mitambo na vifaa vingine vya kisasa vyenye uwezo wa kuendesha Matamasha na mashindano ya Urembo kwa kiwango cha hadhi ya nyota tano.

Wengi wa washiriki hao walionyesha hamasa na kujaribu kuwashawishi viongozi na wakuu wa msafara wao ili kufanya Fainali hizo katika Ukumbi huo ambao umekuwa ni kivutio kikubwa, jambo ambalo Viongozi na kamati iliokuwa na jopo la msafara huo lilionekana kukubaliana na mawazo ya nia ya warembo hao ya kuomba Fainali hizo zifanyike ndani ya Ukumbi huo. 

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Rais wa Mashindano hayo nchini na Barani Afrika Erasto G. Chipungahelo,kuhusu uwezekano wa kuandaa Fainali hizo katika Ukumbi huo wa kimataifa wa NATIONAL MUSIUM THEATRE,  alisema kuwa kila jambo ni mipango, hivyo na kwa kuwa lengo na nia ya Mashindano ya Miss Utalii ni kutangaza Vivutio vya Taifa kuna uwezekano pia Fainali hizo zikafanyika hapo ikiwa pia ni kuwapa heshima Wizara ya Maliasili na Utalii ambao ndiyo walezi wakuu wa mashindano ya Miss Utalii Tanzania kwa kuwa wao ndiyo wamiliki wa Ukumbi huo ambao kwa sasa unaonekana kuwa ni kati ya kumbi pekee zilizojengwa kisasa na hadhi ya kimataifa hapa nchini Tanzania.

ziara hiyo ya kutembelea Ukumbi huo kwa washiriki wa Miss Utalii Tanzania  2012/2013 iliandaliwa na Washiriki wenyewe baada ya kuusikia sifa zake kutoka kwa watu mbalimbali na Mitandao ya Kijamii.

 Aidha Chipungahelo amesema kwamba warembo hao wanatarajia kupanda katika jukwaani baada ya kutoka kwenye ziara ya kutembelea hifadhi za Taifa ambazo ni pamoja na Saadan, Mikumi, Udzungwa, Mkomanzi, Arusha na Mlima Kilimanjaro watakaokuwa wameambatana na waandishi wa habari.

Akizungumzia hali ya Ukumbi  huo Rais wa Miss Utalii Tanzania, Gideon Chipungahelo amesema kwamba ni heshima kubwa kwa Taifa na sekta nzima ya Utalii kuona Warembo ambao wanatangaza Utalii wa Nchi yetu wakivutiwa  na ukumbi huo hata kufikia kupeleka maombi ya kutaka wao kuwa Warembo wa kwanza kupanda katika jukwaa hilo la Ukumbi wa kisasa na wa kimataifa wa NATIONAL MUSIUM  THEATRE ulipo ndani ya Makumbusho ya Taifa ambao ni kivutio kikubwa kwa sasa katika anga za Burudani na sanaa.

“Ukumbi ni mzuri kama ambavyo wenyewe wandishi mlivyoona na kutazama, hakika ni jambo la kujivunia na kusifiwa kwa Wizara yetu, maana unaonekana ni jambo la kujipanga hadi kuweza kutengeneza kwa ubora huo unaoonekana sasa, bila shaka nyie wenyewe mtaona ni kwa kiasi gani Umeandaliwa, lakini hata hivyo ni changamoto kwa Wizara zingine katika kubuni na kuweka rasilimali kama hizi kwa manufaa ya Taifa, kama ambavyo mnaona wenyewe, kwani hata Washiriki wamefurahi na hata kusifia sana hivyo pia nachukua fulsa hii kuishukuru Wizara kwa kuwekeza Ukumbi wa Kisasa ambao ni faida kwa Taifa” alisema Chipungahelo.

Pia aliendelea kusisitiza na kuomba wadau na wapenzi mbalimbali wa mashindano haya kujitokeza kuunga mkono kudhamini na kununua tiketi siku ya shindano..
Erasto G. Chipungahelo
Rais – Miss Tourism tanzania Organisation

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...