Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Thursday, March 21, 2013

WAGUNDUZI GUNDUENI VITU VITAKAVYOWASAIDIA WANANCHI KATIKA JAMII: DK. MWERE



Watafiti na wanasayansi nchini Tanzania wametakiwa kufanya tafiti za kiungunduzi ambazo zitaleta manufaa na kusaidia jamaii ya watanzania .

Hayo yamesema na leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dr. Mwele Malecela(pichani juu) wakati wa semina ya siku moja ya wagunduzi mbalimbali iliyoandaliwa kwa pamoja kati ya NIMR na Shirika la Grand Challenges la nchini Canada.

Dkt. Malecela amesema umefika wakati sasa kwa wagunduzi mbalimbali wa Kitanzania kuanza kungundua njia mbalimbali za kuweza kutatua matatizo yaliyopo katika jamii hasa katika sekta ya afya.

Semina hiyo ya siku moja ilikuwa na lengo la kuhamasisha wangunduzi sekta ya afya ambapo baadhi ya wanasayansi wagunduzi kadhaa walitoa taarifa zao za awali za namna ya kukabiliana na matizo kadha hasa kwa Mama na mtoto.
Wagunduzi kadhaa waliweza kuzungumzia gunduzi zao katika semina hiyo na miongini mwa hizo ni pamoja na ile ya hali ya Utapiamlo unaofanywa na Dkt. Magreth Kagashe kutoka Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Bianadamu Ifakara ambayo inafanyika katika Vijiji vya Kilombero.

Ugunduzi mwingine ni wa namna ya kusafisha maji na kuyaweka katika hali salama kupitia njia ya Takasa maji, na kuyaweka taika hali salama nay a usafiugunduzi unaofanya na Kijakazi Mashoto na Ugunduzi mwingine ni matumizi ya Maua ya Rosella katika kukabiliana na Upungufu wa damu kwa mama na mtoto.

Dkt. Malecela amesema ya kuwa ugunduzi unaofanyika sasa na kupewa fedha na Grand Challenge ya Canada unatakiwa uwe ugunduzi ambao utaleta mabadiliko na kubadili maisha ya wananchi.

“Mara nyingi wanasayansi wamekuwa wakifanya tafiti mbalimbali na kugundua matatizo mengi katika jamii lakini mara chache watafiti hawa wametafuta suluhisho ya hayo matatizo au magonjwa katika jamii hizo ...kwahiyo hivi sasa wanasayansi wagunduzi wa kitanzania umefikia hatua ya kugundua vitu ambavyo vitasaidia jamii,” alisema Dkt.Malecela.

Aidha nae Afisa Mtendaji Mkuu wa Grand Challenge Canada, Peter Singer alisema kuwa jumlya ya miradi 16 ya ugunduzi inayofanywa na wanasayansi wa kitanzania itapatiwa fedha kupitia taasisi hiyo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Grand Challenge Canada, Peter Singer akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya semina hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya NIMR jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dr. Mwele Malecela akipiga picha na Afisa Mtendaji Mkuu wa Grand Challenge Canada, Peter Singer mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari Makao Makuu ya NIMR jijini Dar es Salaam leo.

1 comment:

  1. KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.الالله صلى الله عليه وسلموعليكوتهله صلى الل

    KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.الالله صلى الله عليه وسلموعليكوتهله صلى الل


    KAMI SEKELUARGA MENGUCAPKAN BANYAK TERIMA KASIH ATAS BANTUANNYA MBAH , NOMOR YANG MBAH BERIKAN/ 4D SGP& HK SAYA DAPAT (350) JUTA ALHAMDULILLAH TEMBUS, SELURUH HUTANG2 SAYA SUDAH SAYA LUNAS DAN KAMI BISAH USAHA LAGI. JIKA ANDA INGIN SEPERTI SAYA HUB MBAH_PURO _085_342_734_904_ terima kasih.الالله صلى الله عليه وسلموعليكوتهله صلى الل

    ReplyDelete

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...