Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Sunday, May 19, 2013

Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA)




                                                      Press Release
TAMASHA la Mastaa chipukizi la mwezi Mei litafanyika tarehe 26 katika ukumbi wa Starlight Hotel kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 10 jioni.

Vikundi vya sanaa vya Kaole, Splendid, Super Shine Taarab, Five Star Modern Taarab pamoja na wasanii mbalimbali wa Bongo Flava, Maigizo,Ngoma, Dansi na Sarakasi wamethibitisha kushiriki tamasha hilo.

Wasanii wakongwe wa bongo flava kama Stara Thomas, Bendi ya Msondo Ngoma na waigizaji wakongwe wa Kaole na Splendid wataonesha umahiri wao katika fani ya sanaa.

Kauli Mbiu ni Kilio cha Msanii, wasanii wote wapendao kushiriki wafike ofisi za Splendid Ilala ili kujisajili.

SHIWATA pia inawapongeza wote walioshiriki tamasha  la Aprili 27 ambako zaidi ya wasanii 300 walishiriki kuonesha vipaji vyao ambako mgeni rasmi mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Wilaya ya Kinondoni, Calist Lyimo aliwaasa wasanii kujituma kuonesha uwezo wao katika kuelimisha jamii.

Pia Shiwata imeupongeza uongozi wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) kwa ushirikiano wao mzuri na kuwaomba viongozi wengine wa bendi za muziki, taarab,vikundi vya sanaa,mapromota,maprodusa na wadau bwote tushirikiane katika matamasha haya ili kujenga ushirikiano wa pamoja.

Maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika ambako wasanii kutoka vikundi mbalimbali wamepiga kambi ya kujifua ili kuonesha ubunifu wao katika tamasha hilo.

Wakati huo huo SHIWATA inatarajia kuhamisha tamasha hilo kwa mwezi Juni kufanyikia mkoa wa Arusha ili kuwapa nafasi wasanii wa mkoa huo nao kuonesha uwezo wao.

Peter Mwenda 
Ofisa Habari wa SHIWATA
0715/0752-222677

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...